Kikosi
hiki cha Prisons kimepambana sana msimu huu kubakia ligi kuu soka
Tanzania bara baada ya kukabiliwa na changamoto nyingi sana, sasa msimu
ujao Mbeya itakuwa na “Mbeya Derby” ambapo mashabiki watakuwa
wanazishuhudia timu hasimu za Mbeya City na Tanzania Prisons katika
dimba la Sokoine jijini humo
Hapa
ni moja kati ya mazoezi ya Mbeya City chini ya kocha Juma Mwambusi
aliyewahi kuifundisha Prisons kwa mafanikioa makubwa, sasa wanaume hao
watakabiliana na Prisons msimu ujao
Na Baraka Mpenja
Baada
ya kupigana kufa na kupona na hatimaye kufanikisha ndoto zao za kubakia
ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, viongozi wa Klabu ya maafande
wa Tanzania Prisons “wajelajela” wa jijini Mbeya wamekaa kikao cha
maandalizi ya kuanza zoezi la usajili ili kuimarisha kikosi chao zaidi.
Katibu mkuu wa wajelajela Sadick Jumbe amiembia MATUKIO DUNIANI kuwa
hapo jana walikaa katika kikao cha klabu ili kutathimi hali ya ligi
ilivyoenda na wapi kikosi chao kilikuwa na mapungufu makubwa ili
kurekebisha.
Jumbe
alisema katika kikao hicho wamekubaliana kuongeza wachezaji hasa sehemu
ya kiungo ambayo ina shida kubwa sana pamoja na ushambulaiji.
“Tumepigana
kufa na kupona, tulijua hatuna uwezo wa kupata nafasi za juu badala
yake tulikuwa tunachungulia kaburi, tulipambana na tumefanikiwa kubaki,
haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na sasa tunajiandaa kufanya usajili
mkubwa ili kuimarisha kikosi chetu”. Alisema Jumbe.
Jumbe
alipoulizwa ni wachezaji gani wanatarajia kuwasajili, aligoma kuwataja
kwa madai kuwa kuna mapapa na dagaa, wao ni dagaa na kama wataanika
majina yao basi wanaweza kufanyia umafia na mapapa ambao
watawanyang`anya nyota wao.
0 comments:
Post a Comment