Na Baraka Mpenja
Baada
ya Simba kutangaza kuwasajili wachezaji watatu kwa mpigo akiwemo
mshambuliaji hatari wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,
Zahor Iddi Pazi aliyekuwa anacheza kwa mkopo JKT Ruvu akitokea Azam fc,
Mlinda mlango wa “Wanankulukumbi” kagera Sugar Andrew Ntala na mlinzi
Issa Rashid “Baba ubaya” kutoka Mtibwa sugar, mwenyekiti wa kamati ya
usajili ya klabu hiyo Keptein Zacharia Hans Hoppe amesema Simba haina
sera ya kuchukua wachezaji kutoka Yanga labda akitokea mzuri, lakini wao
wanahangaika kuwachukua wachezaji wa klabu hiyo.
Poppe ameimabia MATUKIO DUNIANI
kuwa Simba mwaka huu wanafanya usajili makini tofauti na mwaka jana na
ndio maana wameanza kwa kuwaongezea mikataba wachezaji wao, kuwapa
vijana wao mikataba na kusajili wapya kama walivyofanya hapo jana.
“Tumewasijili
watatu jana, wengi watajiuliza kwanini tumemchukua kipa Ntala, kiukweli
hatuna pengo safu ya makipa, tunao wazuri lakini tumeona vyema kuongeza
kipa ili apate uzoefu zaidi kwani siku zinaenda”. Alisema Poppe.
Poppe
aliongeza kuwa sera yao ya kimya kimya katika usajili bado inaendelea
huku akiweka wazi kuwa wanataka kuongeza wachezaji wawili wa kigeni
akiwemo beki wa kati na mshambuliaji wa kati ili kuimarisha sehemu hizo
ambazo mwalimu amependekeza zitafutiwe nyota wa kuimarisha.
Kuhusu
Beki Issa Rashid, Poppe alisema Simba kwa sasa haina beki wa kushoto
kwa sasa kwani wanaocheza kwa sasa yaani Haruna Shamte ni beki wa kulia
na Paul Ngalema ameomba kusitisha mkataba wake na Simba.
Kuhusu
Zahor Pazzi Poppe alisema kwa siku nyingi wamekuwa wakimtaka kwa siku
nyingi kwani awali walikuwa na mkataba wa miaka minne naye lakini kuna
mambo yalitokea na kufanya wampoteze.
Poppe
amesema Simba SC wanasajili kisayansi na si kama wapinzani wao hao,
Yanga SC ambao wanaingia hasara ya fedha nyingi na wanacheza pata potea.
“Sisi tulimsajili Mbuyu Twite kama yeye tu, lakini wao wakaingilia akawapa sharti wamsajili na ndugu yake (Kabange Twite), wakaingia mkenge wakasajili mtu ambaye wamemlipa fedha nyingi, lakini hawajamtumia na hakuwa chaguo lao,”.
“Sisi tulimsajili Mbuyu Twite kama yeye tu, lakini wao wakaingilia akawapa sharti wamsajili na ndugu yake (Kabange Twite), wakaingia mkenge wakasajili mtu ambaye wamemlipa fedha nyingi, lakini hawajamtumia na hakuwa chaguo lao,”.
Kuhusu suala la Niyonzima, Poppe alisema Yanga wameingizwa mkenge kwa kumlipa dau nono wakiwa na hofu ya Simba kumsajili.
“Niyonzima
ni mchezaji wao, sisi hatujawahi kuongea nae kama tunataka kumsajili,
nasikia wamempa hela nyingi baada ya kusikia fununu za sisi kumsajili,
hatukuonge nae hata kidogo” alisema Poppe.
0 comments:
Post a Comment