Mahmoud Ahmad Arusha
Waziri mkuu Pinda kukabidhi Madawa
yenye thamani ya tsh.16.2 milion kwa Hospitali ya mkoa mount Meru
wakati atakapowatembelea wagonjwa walipata majeruhi kwenye muendelezo
uliotokea jana wa mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu
JosephMfanyakazi eneo La olasiti Nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Akizungumza wakati akitoa
Mablanketi kwa niaba ya wizara ya utalii kupitia shirika la hifadhi la
taifa (TANAPA)Naibu waziri wa Maliasili na utalii Lazaro Nyalandu
alisema kuwa wizara yake kupitia Tanapa wametoa vifaa hivyo ili kusaidia
hospitali hiyo yenye huba wa madawa na vifaa mbali mbali ikiwemo
upungufu wa vitanda,madawa na mablanketi ambayo sehemu ya madawa
itakabidhiwa jioni na Mh.waziri mkuu kwa niaba ya serekali.
“Kwanza tunatoa pole kwa majeruhi
wote waliopatwa na tukio hilo na tunawatakia wapone haraka pili msaada
huu tunautoa kwa ajili ya kupunguza upungufu uliotokea kwenye hospitali
yetu ntakaa na wenzangu wadau wa utalii tuangalie nini cha kufanya”
alisema nyalandu.
Alisema kuwa jumla ya tsh.16.2
milion zitatumika kununulia madawa ambayo ya takabidhiwa jioni na waziri
mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.
Wakati huo huo kijana wa miaka 16
mkazi wa Olasiti James Gerald amefariki dunia usiku wa kuamkia Leo
ikiwa ni mtu wa pili kufariki katika tukio la mlipuko wa bomu uliotokea
kwenye kanisa la Joseph Mfanyakazi kwenye kata ya Olasit jijini Arusha,
Akithibitisha kutokea kwa mauti
hayo Kaimu mganga mkuu wa Hospitali ya Mount Meru dkt.Mariam Murtazah
alisema kuwa hospitali hiyo ilibidi kuongeza dawa kutokana na wingi wa
watu na kuwa msaada waliupata umekuja wakati muafaka kwani hospitali
hiyo inakabiliwa na upungufu wa vifaa yakiwemo madawa.
Aidha Askofu mkuu wa JImbo kuu la
katoliki Arusha Josephat Lebulu Akiongozana na Balozi wa Vatikan hapa
nchini Fransisco Padilla waliwatembelea majeruhi wa mlipuko wa mabomu
majra ya saa 11;39 na kuwafariji majeruhi hao kwa kuwawekea mkono wa
Baraka kwenye mapaji ya uso.
Akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kutoka kuwatembelea majeruhi hao alisema wamepata salamu
mbali mbali kutoka mataifa mbali mbali wakiwatakia majeruhi hao wapone
haraka na rambi rambi kwa wafiwa huku akitoa tamko la kanisa kuwa ni
mafundisho ya bwana yesu kuwa tuushinde ubaya.
Lebulu aliwataka wakirsto hapa
watanzania kuweka ulinzi wao moyoni badala ya kutegemea polisi kwani
majaribu ya shetani ni mengi kama unavyoona shetani anatumia watu kupiga
mabomu hadi kwenye nyumba za ibada,hata ukiweka ulinzi kwenye nyumba za
ibada bado shetani ataendelea kuwatumia wafuasi wake.
“Tuweke ulinzi rohoni mwetu
kwanza kabla ya kuuweka mbele ulinzi wa Askari wetu hakika kama
hatutatumika na shetani basi matukio kama haya yatakuwa historia”alisema
Lebulu mbele ya balozi Padilla
0 comments:
Post a Comment