Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Miamba
ya soka la Hispania, Real De Madrid imetangaza vita kwa timu
zinazomkodolea macho mshambulijai nyota wa klabu hiyo, Mreno Cristiano
Dos Santos Aveiro Roldo ili zimsajili msimu wa majira ya joto ya usajili
barani ulaya mwaka huu.
Rais wa Real Madrid
Florentino Perez amesema ili kuhakikisha wanazipiku timu zote hasa timu
yake ya zamani ya Manchester United, wanaandaa dau nono la kumlipa
nyota wao ili awe mchezaji anayelipwa vizuri zaidi duniani.
Hii
imetokea siku chache baada ya Mreno Jose Mourinho kutangaza kuihama
klabu hiyo huku akidaiwa kutimka na Ronaldo kwenda naye Chelsea.
“Napenda
kuona Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kulipwa dau nono duniani.
Tunajiandaa kufanya kila linalowezekana kumlipa mshahara mkubwa ili
aendelee kuwa na furaha klabuni kwetu”. Alisema Perez.
Nyota
huyo wa zamani wa Manchester United anatajwa kurudi katika klabu yake
ya zamani ya United, pia anahusishwa na kuhamia PSG ambao wametangaza
kitita kikubwa zaidi kwa mchezaji huyo.
Licha ya kuwepo kwa maneno yote
hayo, leo hii Perez ametangaza vita na amesisitiza Madrid itavunja benki
na kumlipa pesa nyingi zaidi kuliko wachezaji wote duniani.
DILI KUBWA KWA MRENO: Rais Perez anajiandaa kuvunja benki ili kumbakisha Ronaldo
NYOTA WA KWELI: Ronaldo anajiandaa kucheza msimu mwingine akiwa na Real licha ya kumaliza msimu bila kutwaa taji lolote
Tangu
Ronaldo ajiunge na Real Madrid mnamo mwaka 2009 kutoka Manchester
United kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 80, ametia kambani mabao 146
katika mechi 135 alizokipiga nchini Hispania.
Wakati
Real wakijipanga kumbakisha Ronaldo, leo Perez amesisitiza kuwa mpaka
sasa hawajui nani atakuwa kocha mpya wa klabu hiyo, lakini suala hilo
litawekwa wazi wiki ijayo huku mchezaji nguli wa Ufaransa na klabu hiyo
Zinedine Zidane akipewa dili la kusaka kocha mpya.
Kazi
ya kwanza kwa Zidane ni kumleta Gareth Bale katika ligi ya La Liga
akitokea katika klabu ya Tottenham Hospur hata kama itawagharimu pauni
milioni 65 potelea mbali.
WENYE
FEDHA ZAO: Perez (juu) na Zidane (chini) wamesema wanataka
kuwaunganisha Ronaldo na Bale katika dimba la Bernabeu ili wapinzani wao
wakione cha moto msimu ujao, wamekubali kumchukua kwa pauni milioni 65
Zidane
amekuwa akihusishwa sana na Real katika masuala ya usajili tangu
astaafu kucheza soka mwaka 2006, na safari hii amepewa Jukumu la
kumpeleka Bale Bernabeu
ANAWINDWA AKALE MAPESA HISPANIA: Bale kwa sasa amegeuka lulu kutokana na uwezo wake wa kufanya mambo makubwa akiwa dimbani
0 comments:
Post a Comment