Na Baraka Mpenja Kwa Msaada wa Sportsmail.com
Nyota
wa watukutu wa London Tottenham Hospur, baada ya kutwaa tuzo ya
mchezaji bora wa chama cha soka England nchini Uingereza na tuzo ya
mwanasoka bora chipkizi, mambo yanazidi kuwa mazuri kwake na anaweza
kutwaa tuzo nyingine ya goli bora za msimu baada ya bao lake kutajwa.
Nyota
huyo amekuwa mhimili mkubwa kwa klabu yake msimu huu na baada ya
kufunga bao katika mchezo wa jumamosi ya wiki iliyopita dhidi ya
Southampton amekuwa mchezaji wa kwanza kuifungia klabu hiyo mabao 20
katika msimu mmoja wa ligi tangu ambapo Jurgen Klinsmann msimu 1994-95
alifanya hivyo.
Bale ameendelea kufanya vizuri msimu huu na hilo juu ni bao lake alilofunga jumamosi ya wiki ilioyopita
Tuzo mbili sio mchezo: Bale ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa PFA na mchezaji bora chipkizi wa chama cha soka England
0 comments:
Post a Comment