Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportmail.com, Soka In Bongo
Sasa
ni nafasi pekee kwa kocha mwenye meneno mengi, mtu maalumu, Mario Jose
Dos Santos Ferlix Mourinho kurejee tena katika ligi ya England msimu
ujao.
Rais
wa Real Madrid Florentino Perez leo ametangaza kuondoka kwa Kocha wao
Mkuu Jose Mourinho kufuatia makubaliano ya pande zote mbili.
Akihutubia
Wanahabari waliojazana, Perez alisema: “Tumeamua kumaliza uhusiano
wetu. Hakuna Mtu aliyefukuzwa kazi, ni makubaliano ya pande mbili.”
Wakiwa
wamebakisha Mechi 2 za La Liga, Real Madrid wako Nafasi ya Pili na
Pointi 13 nyuma ya Mabingwa FC Barcelona na Ijumaa iliyopita walitwangwa
2-1 kwenye Fainali ya Copa del Rey na Mahasimu wao Atletico Madrid.
MOURINHO
NA MATAJI:UCL: 2004 (Porto), 2010 (Inter Milan), UEFA CUP: 2003
(Porto), BPL: 2005, 2006 (Chelsea), FA CUP: 2007 (Chelsea), LEAGUE CUP:
2005, 2007 (Chelsea), LA LIGA: 2012 (Real Madrid), COPA DEL REY: 2011
(Real Madrid), SERIE A: 2009, 2010 (Inter Milan), COPPA ITALIA: 2010
(Inter Milan), PRIMEIRA LIGA: 2003, 2004 (Porto), TACA DE PORTUGAL: 2003
(Porto)
Katika
Miaka mitatu aliyodumu Real, Mourinho alishindwa kuivusha Real zaidi ya
Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kutolewa katika hatua hiyo
katika Misimu yote hiyo na Msimu huu ilishikishwa adabu na Borussia
Dortmund kwa kuchapwa Bao 4-1 huko Germany na wao kujitutumua na
kushinda 2-0 Nyumbani kwao.
Kabla
Mourinho kutua Real Madrid, Klabu hiyo ilikaa Miaka miwili bila Taji
lolote na alipofika yeye wakatwaa Copa del Rey Mwaka 2011 na kufuatia
Ubingwa wa Spain wa La Liga Mwaka 2012 lakini Msimu huu ametoka patupu
ukiachia Super Cup.
Inaaminika
Jose Mourinho anarudi Klabu yake ya zamani huko England, Chelsea, na
hapo Real atatua Carlo Ancelotti kutoka PSG ingawa haujapatikana
uthibitisho rasmi mbali ya PSG kumkatalia Ancelotti kuhama.
MTU
MAALUMU: Jose Mourinho ameachishwa kazi Real Madrid ana sasa anarudi
Chelsea kwa raha zake. Furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo yenye makazi
jijini London
Mourinho alipooneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa fainali ya Copa Del Rey ambapo alipoteza mabao 2-1 dhidi ya Atletico.
Rais Perez anategemea kumteua kocha wa Paris Saint-Germain Carlo Ancelotti ili achukua mikoba ya Jose Mourinho.
“Lazima
tumshukuru Mourinho kwa kazi nzuri na kujituma zaidi, katika miaka
mitatu aliyokaa hapa, ameifanya timu iwe bora sana, tunamkatakia kila la
heri”. Alisema Perez leo hii.
ANABEBA MIKOBA: Kocha wa PSG Carlo Ancelotti anatajwa kurithi mikoba ya Jose Mourinho
NJOO NYUMBANI: Mourinho kurudi Chelsea itakuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo wanamuota kila siku
Florentino
Perez akiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo hii: “Lazima
tumshukuru Mourinho kwa kazi nzuri na kujituma zaidi, katika miaka
mitatu aliyokaa hapa, ameifanya timu iwe bora sana, tunamkatakia kila la
heri”. Alisema Perez leo hii.
Cristiano Ronaldo anasemekana anaweza kuambatana na Mourinho Chelsea, lakini United nao wanatajwa kumrejesha nyota huyo
0 comments:
Post a Comment