Na Gervas Mwatebela kwa msaada wa Mtandao
Wakati timu ya Barcelona ya Hispania ikitaraji kushuka ugani usiku wa leo kupambana na Bayern Munich ya Ujerumani katika mechi ya marejeano ligi ya
mabingwa Ulaya imekiri kuwa kutinga fainali kunategemea ubora wa Messi siku
hiyo.
Katika mechi ya awali miamba hiyo ya Catalunya iliambulia kichapo cha
magoli 4 – 0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa dimba la Allianz Arena.
Kocha msaidizi wa BARCA Jordi Roura amesema afya ya mchezaji huyo imekuwa
ikiimarika lakini anaamini atakuwa fiti kwa mchezo huo utakaochezwa katika
uwanja wao wa nyumba NOU CAMP.
‘messi ni mchezaji bora duniani hivyo asipokuwepo dimbani utaona tofauti
na akiwepo dimbani utajua utofauti wake’.
Kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kwa Messi katika mchezo uliopita dhidi ya
Bayern Munich ni miongoni mwa kinga kwa makocha wa Barcelona kupoteza mechi
hiyo.
BARCA watahitaji ushindi wa magoli 5
- 0 ili kufuzu fainali ushindi wa magoli 4 - 0 katika dakika 90 utawapeleka
dakika 30 za nyongeza ikishindikana hapo ni changamoto ya mikwaju ya penati
kuamua mshindi.Lionel Messi na Xavi Hernandez wamekiri ugumu uliopo katika
kubadili matokeo hayo.
0 comments:
Post a Comment