Na Gervas Mwatebela kwa msaada wa Mtandao
Ni wazi sasa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya linaelekea Ujerumani
baada ya klabu za nchi hiyo kutinga hatua ya fainali,ambapo Bayern Munich
imeandika historia kwa kuichapa Barcelona kwa magoli 3 – 0 na kusonga mbele kwa
jumla ya magoli 7 – 0 ukijumlisha na
magoli 4 – 0.
Magoli ya Bayern Munich yamefungwa na Arjen Robben,goli la kujifunga la
beki Gerard Pique na Thomas Mueller yalitosha kuifikisha fainali timu hiyo
bingwa wa mara nne wa michuano hiyo kwenda kupambana na ndugu zao Borussia
Dortmund ambao waliwaondosha mabingwa wa mara tisa wa michuano hiyo Real Madrid
kwa jumla ya magoli 4 – 3.
Barcelona ilitakiwa kushinda magoli 5 – 0 ili kutinga fainali itakayochezwa katika dimba
la Wembley,London Uingereza.Sasa Barca
wameungana na ndugu zao Real Madrid ambao licha ya ushindi wa magoli 2 – 0 dhidi
ya Borussia Dortmund ya Ujerumani hayakutosha kuwavusha hatua ya fainali.
Kocha Bayern Munich afichua siri ya ushindi
Kocha
Jupp Heynckes wa Bayern
Munich amesema siri ya ushindi wa timu yake dhidi ya Barcelona ya Hispania ni
kwa sababu vijana wake wana uwezo na wanalijua soka la klabu za Hispania.
Kocha
huyo mwenye umri wa miaka 67 amesema kuwa analifahamu vyema soka la Hispania na
falsafa ya klabu ya Barcelona hivyo anawapongeza vijana wake kufuata maelekeza
na kuwatupa nje ya michuano klabu ambayo imekuwa tishio kwa takribani miaka
nane iliyopita.
‘Nalifahamu
soka la kihispaniola,nawajua wachezaji,naifahamu falsafa ya Barcelona,huwa
napenda kuangalia mechi za EL CLASSICO yaani Barca ikipambana na Real Madrid
huwa naburudika sana.’alisema kocha Jupp.
Jupp Heynckes akishangilia ubingwa |
Kocha
huyo ambaye aliiwezesha Real Madrid kutwaa kombe hilo mwaka 1998 amesema klabu
yake inacheza kitimu soka la kasi na lenye malengo ya ushindi ndiyo siri ya
mafanikio.
Kocha
huyo mbali ya ushindi dhidi Barcelona,pia timu yake ililazimika kuvuka viunzi
kadhaa ikiwemo kuitupa nje Arsenal ya England katika hatua ya 16 bora kisha
ikawafurusha mashindanoni vinara wa ligi kuu Italia Juventus katika hatua ya
Robo fainali.
LIONEL MESSI
HAYUKO FITI KABISA-VILANOVA
Kocha wa Barcelona ya Hispania Tito Vilanova amesema alimuweka nje ya dimba nyota wake Lionel Messi
katika mechi ya marejeano dhidi ya Bayern Munich kwa sababu hayuko fiti.
Katika mechi hiyo ya nusu fainali ya pili ambapo Bayern Munich
waliwanyanyasa wenyeji wao kwa kuwapiga magoli 3 – 0 hivyo kusonga mbele kwa
jumla ya magoli 7 – 0 kwani katika nusu fainali ya kwanza Bavarians walishinda
kwa magoli 4 – 0.
Kocha huyo amesema kuwa Messi asingeweza kucheza katika mechi hiyo lakini
amekanusha kuwa utegemezi wa BARCA kwa muargentina huyo umesababisha timu hiyo
kutolewa katika ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Kocha huyo amesema kuwa Bayern
Munich walikuwa bora karibu kila idara kwa mechi zote mbili kuanzia dimbani na
kisaikolojia walitimia ndiyo sababu wametinga hatua ya fainali ya ligi ya
mabingwa Ulaya.
Kocha huyo amesema kutokuwepo kwa Lionel Messi,Carles Puyol,Eric Abidal
na Sergio Busquets siyo kisingizio kwa timu yake kutolewa katika michuano hiyo.
TITO VILANOVA |
0 comments:
Post a Comment