MBUNGE
wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani (CCM), amesema kuwa yuko tayari
kujiuzulu ubunge endapo madai yanayotolewa na wapinzani wake wa kisiasa
kuwa amekuwa akifadhili genge la wahuni kuendeleza mgogoro wa Wakulima
na Wafugaji.
Akizungumza
na FULLSHANGWE kwa njia ya simu jana, Ngonyani (Profsa Maji Marefu),
alisema wema wake katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo kwenye kijiji
cha Magamba kwa Lukonge ndio unaomponza.
Alisema
kunakikundi cha baadhi ya wafugaji ambao ndio chanzo cha mgogoro huo
tangu miaka 15 iliyopita kuwa wamejipanga kwenda kumshtaki kwa rais
Jakaya Kikwete mbunge huyo kutokana na kupendelea upande mmoja.
“Mimi
nilikuwa mstari wa mbele katika kusimamia mgogoro huo ili wananchi hao
waweze kuishi kwa amani na mimi nimechaguliwa na wananchi wote wafugaji
na wakulima sasa itakuwa ajabu kuukandamiza upande mmoja hii si tabia
yangu”alisema.
Ngonyani
alisema kutokana na mgogoro huo ambao umekuwa ukichochewa na baadhi ya
wanansiasa aliowashinda kwenye uchaguzi mwaka 2010, yuko tayari
kujiuzulu ubunge endapo madai hayo yanayopelekwa kwa Rais yakithibitika
yana ukweli.
“Hivi
karibuni wakati nikiwa bungeni nilipata taarifa kuwa kuna mfugaji
aliingiza ng’ombe wake kwenye shamba la mkulima lenye heka sita ambako
ng’ombe hao waliharibu mazo yote kitendo kilichozua vurugu”alisema.
Kutokana
na hali hiyo, ilimbidi kurudi jimboni kwake kwa ajili ya kutafuta
ufumbuzi ambapo alikutana na Mkuu wa Wilaya pamoja na pande zinazohusika
kutafuta ufumbuzi wa kumaliza mtafaruku huo.
Katika
hali ya kushangaza kuna taarifa zilizoandikwa na gazeti moja (si hili),
kuwa yeye alkuwa akikifadhili genge lililojulikana kama ‘Mungiki’
kuwafanyia vurugu wafugaji kitendo mbacho si kweli.Aliongeza kuwa
haitatokea kuungana na watu wanaoendesha vurugu katika jimbo hilo
vilevile aliwataka baadhi ya wanasiasa kuacha kudumisha migogoro kwa
ajili ya kujipatia umaarufu.
0 comments:
Post a Comment