Muuguzi
wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Sr. Felista John
(katikati aliyevaa gauni jeupe) akipokea msaada wa vyakula mbalimbali
kutoka Meneja Uendeshaji Mikopo wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),
Mwanaisha Ayosi, iliyotolewa na benki hiyo kitengo cha Operesheni ikiwa
ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii
hospitalini hapo. Wengine ni wafanyakazi katika kitengo hicho.
Mmoja
wa wafanyakazi wa maofisa wa benki ya NBC, Lioba Massao (kushoto)
akifanya maombezi kwa baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika wodi ya
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) katika hafla ambayo benki
hiyo kitengo cha operesheni kilikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali
ikiwa ni moja ya mikakati ya benki hiyo kusaidia shughuli za kijamii
hospitalini hapo. Baadhi
ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa
katika taasisi hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za
vyakula.
Baadhi
ya wafanyakazi wa NBC wakimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa
katika taasisi hiyo na pia kumkabidhi msaada wa sabuni ya kufulia.
Baadhi
ya wafanyakazi wa NBC wakibeba mizigo ya vyakula na mafuta ya kupikia
tayari kuwakabidhi wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road ya jijini Dar es Salaam kama sehemu ya juhudi za NBC katika
kusaidia shughuli za jamii.
0 comments:
Post a Comment