KLABU ya Napoli inajiandaa kukubali
kumchukua Edin Dzeko kama sehemu ya dili la kumtoa Edinson Cavani kwenda
Manchester City mwishoni mwa msimu.
Mshambuliaji huyo wa Uruguay mwenye umri
wa miaka 26, ana thamani ya Pauni Milioni 53 na pia anatakiwa na vigogo
wa Hispania, Real Madrid.
Ikiwa Dzeko atakwenda Italia kama sehemu ya dili hilo dau la Cavani litapungua hadi Pauni Milioni 35, kwa mujibu wa gazeti la Mirror.
Cavani amekuwa na msimu mzuri na Napoli -
akifunga mabao 23 katika mechi 29 za ligi alizoichezea klabu yake,
lakini nje ya Uwanja anakabiliwa na matatizo binafsi.
Ndoa yake iko shakani, baada ya kudaiwa
kuinfgia kwenye mahusiano ya nje na binti wa miaka 22, Stefania Fummo
ambaye ni mwanafunzi.
Mke wake, Soledad Cavani amesema: "Edinson amemsaliti Mungu. Amenisaliti mimi na mtoto wake, lakini bado nampenda,".
Mtu wa kuchungwa: Cavani amekuwa hatari mbele ya mdomo wa lango msimu huu
0 comments:
Post a Comment