Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportmail.com
JUMAPILI,
MEI 19, ni Siku ya Mwisho ya Msimu 2012/2013 wa ligi kuu soka nchini
England “Barclays Premier League”, na Siku hiyo ndio Mechi ya 1500 kwa
Mscotish Sir Alexndar Chapman Ferguson “Kibabu Fergie” akiwa Meneja wa
mashetani wekundu, Manchester United na ndio mwisho wa enzi yake kwa
vile anastaafu baada ya mechi hiyo.
Sir
Alex Ferguson, Miaka 71, amenena: “Ni Mechi ya 15oo, ni mechi yangu ya
mwisho, hakika inashangaza! Nataka kushinda hii kupita ile ya Wiki
iliyopita!”
Leo,
kwenye Mkutano na Wanahabari kwenye Kambi ya Mazoezi ya Man United huko
Carrington ambao ni kawaida ya kila Ijumaa kabla Mechi za Wikiendi,
Wanahabari walimpa Sir Alex Ferguson zawadi ya Keki yenye umbo la
Mashine ya Kukaushia Nywele ukiwa ni mzaha kuhusu imani ya kwamba Meneja
huyo huwapa kibano Wachezaji wake wasipofanya vizuri na kuwafanya
wajisikie vichwa vyao moto mithili ya kupitishiwa Mashine hiyo ya
Kukaushia Nywele.
Akijibu
kwa mzaha, Ferguson alisema: “Inastahili! Kuna wakati sikukubaliana
nanyi na kile kilichoandikwa na kuna wakati mliandika vitu vizuri tu na
nilividharau. Lakini Siku zote sikuweka kinyongo wala kisasi. Hiyo si
staili yangu!”
Ferguson
pia alithibitisha kuwa Kipa Anders Lindegaard atakaa Golini Mechi na
WBA na Masentahafu watakuwa Jonny Evans na Phil Jones huku Nemanja Vidic
na Rio Ferdinand wakiwa Benchi akisisitiza sasa ni zama za Vijana
Jumapili
iliyopita Sir Alex Ferguson aliagwa kwa shangwe walipocheza Mechi na
Swansea City Uwanjani Old Trafford, ikiwa ni Mechi yake ya mwisho
Uwanjani hapo, na kushinda Bao 2-1 na Jumatatu Timu nzima ya Man United
ilitembeza Kombe la Ubingwa wa BPL kwenye Mitaa ya Manchester na
kusindikizwa na Maelfu ya Washabiki hadi katikati ya Jiji, eneo la
Albert Square, walipopokewa na Maelfu ya Umati.
Mwenyewe
Ferguson amekiri kuwa mapokezi ya Wiki iliyopita yalishinda yale ya
Mwaka 1999 walipopita Mitaani baada ya kutwaa Trebo, yaani Ubingwa wa
England, FA CUP na UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na kuweka Historia ya kuwa
Klabu ya kwanza na pekee Uingereza kufanya hilo.



Daah! si mchezo: Ferguson anastaafu kuifundisha United baada ya kukaa na timu kwa miaka 27 akiwa kocha mkuu

Kibabu akifurahia tu, hana shida kwa sasa

Ferguson
aliwaongoza wachezaji wake kupita mitaa mbalimbali ya jijini Manchester
kushangilia ubingwa wake wa 20 jumatatu ya wiki hii

MIAKA YA NYUMA: Huu ni ubingwa wa United wa mwaka 1999 ambao Fegie alitwaa

Kipato huleta majivuno, nini cha kumnyima raha kibabu?, kafanikiwa kila kona akiwa na United
0 comments:
Post a Comment