Na Baraka Mpenja
Mwamuzi
atakayeshika kipenga katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la
dunia mwakani nchini Brazil kati ya timu ya taifa ya Tanzania “Taifa
Stars” dhidi ya Simba wa milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco
amewekwa hadharani.
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika
Kusini anayejulikana kwa jina la Fraser Daniel Bennett.
Mechi
hiyo ya kundi C itapigwa juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco
kwenye Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku kwa saa za Morocco.
Bennett
atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi
msaidizi namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka Kenya. Mwamuzi wa
akiba (fourth official) ni Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.
Kamishna
wa mechi hiyo ni Robert Mangollo-M’voulou wa Gabon wakati mtathimini wa
waamuzi (referee assessor) ni Charles Masembe kutoka Uganda.
Taifa
Stars ambayo iko chini ya Kocha Kim Poulsen, na ikidhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini katika hoteli ya Tansoma
ikiendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo ambapo kabla itajipima na
Sudan (Nile Crocodiles) Juni 2 mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Ratiba ya mazoezi kwa timu hiyo ni kama ifuatavyo;
Mei 22 Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 23 Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 25 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni Uwanja wa Karume
Mei 26 Saa 3 asubuhi Uwanja wa Karume
Katika
mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, Taifa
stars iliifunga Morroco mabao 3-1 huku mabao mawili yakitiwa kimiani na
Mtanzania Mbwana Samata anayekipiga TP Mazembe ya DRC Kongo na bao moja
likifungwa na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe.
Kabla ya
mechi hiyo, kocha wa stars Mdenimark Kim Paulsen alisafiri kwenda nchini
Afrika kusini kuona mechi za kombe la mataifa ya Afrika ambapo Morroco
na Ivory Coast, wapinzani wa stars walishiriki na mwalimu kuwasoma
vizuri sana.
Stars
wakitoka Morroco watacheza na Ivory Coast uwanja wa taifa jijini Dar es
salaam wakihitaji kufuta kipigo cha mabao 2-0 walichoambulia jijini
Abijan nchini Ivory coast mwaka jana.
Baada ya
kumaliza kipute hicho Stars itawafuata Gambia nyumbani kwao huku ikiwa
na kumbukumbu ya kuwatungua mabao 2-1 uwanja wa taifa jijini Dar es
salaam.
Stars ipo kundi C na mpaka sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 6 nyuma ya Ivory Coast wenye pointi 7 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment