Na Baraka Mpenja
Viongozi
wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013,
“Kwalalumpa Malysia” Dar Young Africans wamesema wanaandaa utaratibu
maalumu wa kusherehekea ubingwa wao wa 24 na wanachama wao.
Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa sherehe zimeanza tangu juzi, lakini wanajipanga kuaandaa siku maalumu kushangiliwa ubingwa wao.
“Watu
hawakulala hata kidogo baada ya kuwafunga Simba, sherehe zile hazitoshi,
sasa tunaandaa sherehe ya pamoja kufurahi kwa pamoja na mashabiki
wetu”. Alisema Mwalusako.
Mwalusako
aliongeza kuwa viongozi wa Yanga wamefurahi sana kutwaa ubingwa kabla ya
ligi kumalizika na kuwatandika watani zao wa jadi mabao 2-0 katika
mechi ya kufunga pazia la ligi kuu msimu huu.
“Waliongea
sana na wakajitapa, mimi nilisema wakati wa meneno umekwisha, tusubiri
siku ya mechi, kweli siku ikafika tukawafunga, ni raha sana kwetu”.
Alisema Mwalusako.
Katibu
huyo alisisitiza kuwa ubingwa wa msimu huu umetokana na sababu nyingi
sana , lakini kubwa zaidi ni ushirikiano mkubwa wa viongozi, mashabiki
na wanachama wa Yanga.
“Viongozi
tumefurahishwa sana na umoja wa mashabiki wetu, angalia uwanja
ulivyofurika mashabiki wa rangi ya kijani na njano, tunawashukuru sana”.
Alisema Mwalusako.
Mwalusako
aliongeza kuwa ubingwa wa msimu huu ndio mwanzo wa mapambano, sasa
wanajipanga kwa ajili ya mashindano ya kimataifa na lazima wafanye
vizuri.
Akiwazungumzia wapinzani wao Simba, Mwalusako alisemanwana timu nzuri na wanacheza vizuri sana.
“Wako
vizuri, lakini hawana ubora zaidi yetu, sisi ni wazuri sana, nafikiri
baada ya miaka mitano ijayo watatufikia kuwa na kikosi bora”. Alisema
Mwalusako.
Wakati
Mwalusako akitamba, naye katibu mkuu wa baraza la wazee wa Yanga,
Ibrahim Akilimali alisema leo hii wanakutana pamoja kufurahi baada ya
kuwafunga Simba.
“Nilisema
lazima mnyama achinjwe, na amechinjwa kwa risasi mbili tu. Alitufunga
tano kwasababu wazee tulivua kofia na safari hii hatukuvua kofia,
matokeo yake wamepigwa kama kawaida, leo tunakutana kufurahi pamoja”.
Alisema Akilimali.
Baada ya
kutwaa ubingwa, sasa Yanga wataliwakilisha taifa katika michuano ya ligi
ya mabingwa barani Afrika ambayo wenzao Simba walitolewa kwa kufungwa
nje ndani na Libolo ya Angola.
Walifungwa bao moja sifuri uwanja wa taifa na wakatandikwa mabao 4-0 nchini Angola.
0 comments:
Post a Comment