Na Mwandishi Wetu
KITABU
cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa
jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya watani wa
Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa
Taifa.
Akizungumza
na jijini jana, mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa
Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela alisema kuwa
maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa na kampuni TSN
Group kupitia kinywaji chake cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events
World, Vannedrick Tanzania Limited na Inbox Pub.
Wadhamini
wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa mujibu wa
Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya
kuuzwa Tanzania nzima. Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia
ya soka la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi
kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali
ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo,
mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano
kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa
miguu Tanzania.
“Pia
nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi
cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa
makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa
kwanza Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
Alisema
kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha,
waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za
mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti
vya timu za taifa na mambo mengine.
0 comments:
Post a Comment