Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
KITABU cha
kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania kijulikanacho kwa jina
la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa leo katika maeneo tofauti ya jiji
la Dar es salaam, lakini siku ya kesho kwenye mechi ya watani wa Jadi,
Yanga na Simba kitauzwa kwa wingi zaidi.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI,
mtunzi wa kitabu hicho, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda
nchini (TFF), na mdau mkubwa wa kandanda Fredrick Mwakalebela amesema
kitabu hicho gharama yake ni shilingi elfu kumi tu (10,000) na tayari
kila kitu kinakwenda sawa.
Mwakalebela alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya kuuzwa Tanzania nzima.
Alisisitiza
kuwa kitabu hiki ni muhimu sana kwa wana-habari, wachezaji, makocha,
waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna kumbukumbu zote za
mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji, vikosi tofauti
vya timu za taifa na mambo mengine.
“Nakala
hizo ni mwanzo tu, nafikiri nitatoa nyingi zaidi ili ziwafikie
watanzania. Hata kwa waandishi wa habari ni muhimu sana kwani kinaweza
kutumiwa kama mrejeo wa matukio mbalimbali ya soka letu”. Alisema
Mwakalebela.
Katibu
huyo wa zamani wa TFF na mdau wa soka la Tanzania aliongeza kuwa kitabu
hicho kimezungumzia historia ya soka la Tanzania katika Nyanja za
vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania Bara, Taifa Cup, Timu
ya Taifa na Utawala Bora.
“Ni kitabu
kizuri sana, hutapoteza pesa yako, kitakupa taarifa nyingi sana pamoja
na kumbukumbu za soka letu, vikosi vya zamani, kauli za makocha
waliopita na mstakabali wa soka letu”. Alisema Mwakalebela.
Mbali ya
hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha Marcio Maximo, mchango wa
serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini, uhusiano kati ya
waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira wa miguu
Tanzania.
“Pia
nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar Tenga kwa kipindi
cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka kwa
makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa
kwanza Juni 15, 2006,” alisema Mwakalebela.
0 comments:
Post a Comment