Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Kocha
mpya wa maafande wa jeshi la kujenga taifa wa mkoani Pwani, JKT Ruvu,
Keny Mwaisabula “Mzazi” kesho anatarajia kuanza mazoezi na kikosi cha
timu hiyo kujiandaa na kipute cha funga pazia la ligi kuu soka Tanzania
bara dhidi ya watengeneza sukari wa Mtibwa Sugar wenye makazi yao
mashamba ya miwa Turiani Mkoani Morogoro.
Mwaisabula ameipasha MATUKIO DUNIANI kuwa
tayari amemwaga wino katika karatasi ya mkataba wa kuwanoamaafande hao
wa jeshi na sasa hesabu zake ni msimu ujao wa ligi kuu unaotarajia
kuanza mwezi wa nane mwaka huu.
“Kimsingi
JKT Ruvu nina mkataba nao, naanza mazoezi mepesi kuwaandaa kwa ajili ya
mchezo wa mwisho dhidi ya Mtibwa, vijana kiukweli ni wazuri sana ila
kuna mambo madogo wanakosa”. Alisema Mwaisabula maarufu kwa jina la
“Mzazi”.
Kocha
huyo mwenye historia ya kuzifundisha timu nyingi wakiwemo mabingwa wa
sasa wa ligi kuu bara, klabu ya Yanga ya Dar es salaam, aliongeza kuwa
kikosi cha maafande hao ni kizuri, wachezaji wanaweza kucheza mpira
lakini wamekosa masaada wa kisaikolijia na hilo ndio jukumu mojawapo
kwake kwa sasa.
“Timu
ni nzuri, natakiwa kuwajenga kisaikolojia ili wajiamini zaidi,
walipatwa na mshituko baada ya Kilinda kuwaacha katika kipindi kigumu,
lakini naamini nitaweza kuwarudisha katika soka la ushindani kama misimu
ya nyuma”. Alisema Mwaisabula.
Mwaisabula
alisisitiza kuwa baada ya msimu huu wa ligi kuu kumalizika atakaa chini
na kuandaa ripoti yake ambayo itajumuisha mapendekezo ya marekebisho ya
kikosi ili aongeze bunduki kali za msimu ujao.
Pia alisema anafurahishwa sana na ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi wa timu hiyo ingawa amekaa kwa muda mfupi.
“Viongozi
wangu Wanaonesha upendo na mshikamano mkubwa kwangu, nitawalipa fadhila
kwa kuunda kikosi kikali cha kushindana msimu ujao”. Alisema
Mwaisabula.
0 comments:
Post a Comment