Na Kibada Kibada-Mpanda Katavi
Katika
hali isiyo ya kawaida mwanamke aitwaye Johari Raphael ( 35) mkazi wa
mtaa wa Makanyagio Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi
amejifungua mtoto wa kiume mwenye viungo vya ajabu utofauti na
banadamu wa kawaida.
Mganga
Mkuu wa Hospital ya Wilaya ya Mpanda Naibu Mkongwa aliwaambia
waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuwa mwanamke huyo alijifungua
mtoto wa ajabu ambae alikuwa na kichwa kikubwa kama cha mtu mwenye
umri mkubwa huku mikono na miguu yake ikiwa mifupi mfano wa pingili
za miwa.
Dkt
Mkongwa alieleza kuwa mwanamke huyo alijifungua mtoto mwenye uzito
wa kilo nne na nusu(4.5) hata hivyo alifariki dunia muda mfupi
baada ya mama yake kujifungua kwa njia ya upasuaji baada ya kushindwa
kujifungua kwa njia ya kawaida katika hospitali hiyo.
Madaktari
waliamua kumfanyia upasuaji baada ya kupata maelezo kutoka kwa mama
huyo alipoeleza kuwa huo ulikuwa ni uzao wake wa tano na kati ya
zao hizo amekuwamara hizo akijifungua kwa shida hali iliyo pelekea
kujifungua watoto wawili wakiwa wameisha kufa.
Dkt
Mkongwa akifafanua zaidi alieleza kuwa baada ya kupata historia ya
mama huyo waliamua kumfanyi a uchunguzi na walipobaini kuwa mama huyo
hawezi kijifungua kwa njia ya kawaida kutokana na ukubwa wa kichwa
alicho kuwa nacho mtoto ambacho mwanamke yoyo hawezi kujifunga kwa
njia ya kawaida
Alisema
kutokana na hari hiyo madakitari wa waliamua kumfanyia upasuaji na
ndipo mtoto huyo wa kiume alipotolewa na alifariki muda mfupi baada ya
kuzaliwa
Kwa
upande wake muuguzi mkuu wa hospital hiyo ya wilaya ya Mpanda Elexzanda
Kasagula alisema kuwa mwanamke huyo alifikishwa katika hospital hiyo
hapo juzi na kulazwa katika wodi ya wazazi baada ya kuonekana muda wake
wa kujifungua umefika
Alieleza
hari ya Johari ambae amelazwa katika wodi ya wazazi inaendelea
vizuri na wanasubiriwa ndugu zake ili wakabidhiwe mwili
wamarehemu kichanga hicho kwa ajiri ya mazishi
Kasagula
alisema hili ni tukio la pili ndani ya kipindi cha miezi mitatu kwa
kuzaliwa watoto wa ajabu kwani miezi mitatu iliyo pita alizaliwa
mtoto huku utumbo ukiwa nje juu t umbo
0 comments:
Post a Comment