Mtaalam wa sheria za kimataifa na Haki za Binadamu kutoka mtandao wa kimataifa wa wabunge wanaotetea Haki za Binadamu, Amani na Utawala wa Sheria duniani Bw. Peter Barcroft (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkutano wa wabunge walio kwenye mtandao huo jijini Dar es salaam kujadili namna watakavyounganisha nguvu zao katika kuzihamasisha na kuzishawishi nchi mbalimbali duniani kupinga na kuzuia silaha kuangukia mikononi mwa makundi ya wahalifu kwa kusaini mikataba inayozuia hali hiyo.
Mbunge
kutoka Ghana Bw. Alban Bagbin akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
kuhusu umuhimu wa mkutano wa wabunge walio katika mtandao wa Kimataifa
wa kutetea amani, maendeleo, utawala wa sheria na Haki za Binadamu
duniani watakavyopanga mikakati mbalimbali ya kuzishawishi nchi
wanazotoka kusaini mikataba inayozuia uagizaji , uingizaji na usambazaji
wa silaha katika nchi zao kuyafikia makundi yasiyohusika ambayo
yamekuwa chanzo cha uvunjifu wa amani duniani. Takribani wabunge 22
kutoka nchi za Afrika wanashiriki mkutano huo.
Mbunge
kutoka Sierra Leone Bernadette LAHAI akiwaeleza waandishi wa habari
(hawapo pichani) athari zinazosababishwa na silaha kuangukia katika
mikono ya wahalifu hasa katika bara la Afrika na kuwa chanzo cha
machafuko na kukwamisha maendeleo ya wananchi.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment