Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha
machachari na mwenye maneno mengi Mario Jose Dos Santos Mourinho
anamkodolea macho mchezaji Kiungo Luka Modric wa Real Madrid ili
aondoke naye kuelekea zake klabu ya Chelsea.
Mourinho
alithibitisha wiki iliyopita kuwa anaondoka Real na anataka mchezaji
huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham kuambatana naye katika safari yake
hiyo ya kuelekea darajani.
Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa ataigharimu Chelsea pauni milioni 30 ili kutia maguu yake darajani.
Habari
za ndani kutoka klabu ya Chelsea zinaeleza kuwa “Mourinho yuko makini
kufuatilia suala la Modric na lazima atue nae darajani, tunajua ni kazi
ngumu sana lakini tunamuamini sana kocha wetu”.
Modric
mwenye miaka 27 hajafanya kubwa sana nchini Hispania, lakini Mourinho
bado amejenga imani kubwa sana licha ya kucheza mechi 31 tu katika msimu
wa ligi kuu ya La Liga.
WANARUDI : Modric na Mourinho wote wanatarajiwa kurudi ligi kuu soka nchini Uingereza League
Mourinho yuko makini kumuwinda Modric ili asepe naye kuelekea Chelsea
Modric amekuwa na msimu mgumu sana Real Madrid lakini Mourinho bado ana imani kubwa sana na nyota huyo raia wa Croatia
Chelsea wana Historia ya kumhitaji Modric na mnamo mwaka 2011 walituma ofa mbili lakini Spurs walizitupilia mbali
ANARUDI: Mashabiki wa Chelsea wameonesha nia ya kumtaka Mourinho darajani
0 comments:
Post a Comment