Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Daah! Ali manusura vijana wa Mourinho waione Wembley mwaka huu baada ya kuwafunga nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani, Borrusia Dortmund mabao 2-0 usiku huu katika dimba la Santiago Bernabeu
Matokeo
hayo yameitupa nje Real Madrid kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza
nchini ujerumani ambapo Mourinho alipiga kipigo cha mbwa mwizi cha mabao
4-1 na baada ya kushinda leo kwa mabo mawili Madrid wanatoka kwa
wastani wa mabao 4-3.
Mchezo
wa leo ulikuwa mgumu sana kwa Mourinho kwani walilazimika kumaliza
kipindi cha kwanza wakiwa 0-0 na kipindi cha pili kilipoanza bado mambo
yalikuwa magumu mpaka dakika ya 83 ambapo waliandika bao la kwanza
kupitia kwa Mfaransa Karim Benzema akipokea pasi nzuri kutoka kwa
Mjerumani Mesut Ozil.
Na
katika dakika ya 88 beki machachari Sergio Ramos alimalizia pasi
maridhawa ya Karim Benzema na kuzamisha gozi kambani, lakini matokeo
hayo hayajafua dafu kufuatia kipigo cha 4-1 ugenini.
Katika
kipindi cha kwanza cha mchezo huo Real Madrid walicheza vizuri zaidi ya
wapinzani wao lakini walishindwa kupangua ngome imara ya Kocha Flopp
aliyetamba toka awali kuwa hawataweza kuwafunga, lakini kipindi cha pili
waliachia na kufungwa, kama Madrid wangekuwa makini wangewatoa leo
baada ya kupoteza nafasi muhimu.
Ozil
hatasaulika kwa mashabiki wa soka wa Real Madrid baada ya kupoteza
nafasi muhimu za kufunga mabao ambayo yangewapeleka dimba la taifa la
Wembley nchini Uingereza kucheza mchezo wa fainali.
Waswahili
wana msemo wao usemao “Mwenzako akinyolewa zako tia maji”, Madrid
safari yao imekwisha leo usiku huku wakiathiriwa na matokeo ya mchezo wa
kwanza, watani zao wa jadi, FC Barcelona nao kesho wanapambana na
Wekundu wa kusini mwa Ujerumani FC Bayern Munich katika dimba la Camp
Nou huku Barca wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 4-0 Allianz
Arena.
Je
yatawafika ya Madrid leo ama watafunga mabao 5-0 ili wafuzu fainali na
hatimaye kukutana na Dortmund ambao wameshakata tiketi leo usiku.
Muuaji Robert Lewandowski akijaribu kupiga mpira kwa utalaamu mkubwa
Sergio Ramos akishangilia bao lake la pili lililowapa Madrid Matumaini makubwa
VIKOSI VYA TIMU ZOTE
Real Madrid: Diego Lopez, Essien, Varane, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Di Maria, Ozil, Ronaldo, Higuain.
Subs: Casillas, Pepe, Khedira, Kaka, Benzema, Albiol, Morata.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender, Blaszczykowski, Gotze, Reus, Lewandowski.
Subs: Langerak, Kehl, Leitner, Sahin, Grosskreutz, Schieber, Felipe Santana.
Mwamuzi: Howard Webb
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Hummels, Schmelzer, Gundogan, Bender, Blaszczykowski, Gotze, Reus, Lewandowski.
Subs: Langerak, Kehl, Leitner, Sahin, Grosskreutz, Schieber, Felipe Santana.
Mwamuzi: Howard Webb
Ramos akitandika mkwaju mkali kwa guu la dhahabu kwa wanasoka, guu la kushoto
: Benzema akiandika bao la kwanza
Wachezaji wa Real
Madrid wakimtaka kipa wa Dortmund Roman Weidenfeller asimame baada ya
kufunga bao la kwanza kwani alionekana kutka kupoteza wakati
Haikutosha: Cristiano Ronaldo hajaweza kuisadia Madrid kufika fainali ya UEFA mwaka huu
Robert Lewandowski akichungulia moja ya mashuti yake kama unaingia kimiani ama la
Hakuna Ujanja: Nyota wa Real Madrids Gonzalo Higuain akijaribu kumpokonya kipa Mats Hummels
Wakiruka juu zaidi: Lewandowski akipigania mpira na beki wa Madrid Raphael Varane
Ronaldo akionekana akilalamika baada ya kuungashwa
Hana jinsi: Mourinho akionekana amepaniki sana
Mwisho wa safari: Ronaldo akitembea uwanjani akionekana amechanganyikiwa na mwenye mawazo baada ya filimbi ya mwisho
0 comments:
Post a Comment