Na Baraka Mpenja
Mnyama
pori, Simba ya Dar es salaam kesho ndio kesho, wanashuka ugani
kuburuzana na maafande wa Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu soka
Tanzania bara uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo
wa kesho unatokana na mechi baina ya timu hizo iliyotakiwa kuchezwa
aprili 25 kuahirishwa kwa kile kilichoadaiwa kuwa uwanja wa taifa
ulikuwa katika matumizi ya sherehe za Muungano aprili 26 mwaka huu.
Taarifa
za kuahirishwa kwa mechi hiyo zilikuja kwa ghafla sana na kuwashangaza
mashabiki wengi wa soka kwani taarifa ilitolewa siku ya mechi na
shiriksiho la soka Tanzania TFF.
Timu
zote zilieleza masikitiko yao kuhusu kuahirishwa ghafla mechi hiyo
kufuatia kukamilisha maandalizi ya mechi hiyo, lakini siku ndio inawadia
ambayo ni kesho uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Kuelekea katika kipute hicho timu zote zimetamba kuibuka na ushindi, huku tambo za mashabiki zikiendelea kila kona ya jiji.
Kocha msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelu “Julio Alberto” ameimabia MATUKIO DUNIANI kuwa maandalizi ya mechi yamekamilika na kikosi chao kipo salama chini ya kocha mkuu Mfaransa Patrick Liewig.
Julio
alisema kikosi cha Mnyama ambacho kimesheheni makinda wengi kitacheza
soka la kitabuni na kuwafurahisha mashabiki wao watakaofurika uwanja wa
taifa.
“Sisi
tunajenga kikosi na tunajua kwamba muda unahitajika, tunamshukuru Mungu
kwa kutupa uzima na kesho tutacheza kutafuta ushindi mnono mbele ya
Shooting ambao ni timu nzuri”.
Julio
aliongeza kuwa siku zote ukitaka kuona raha ya soka ukutane na Ruvu
Shooting ya Mkwasa kwani wanacheza soka safi na hapo kesho watakutana
wataalamu wa soka na kutoa burudani maridhawa.
Wakati
Julio akitamba kuwafunga Shooting, maafande hao kupitia kwa afisa
habari wake Masau Bwire wamesema kuwa kauli ya Simba kuwa wanataka
kulinda heshima yao kesho itagonga mwamba kwani watachinjwa tu.
Masau
alisisitiza kuwa wamejiandaa kwa uzuri sana na wanajua Simba wana
machungu ya kupoteza ubingwa na kuelekea kukosa nafasi ya pili, lakini
wamejipanga kupambana nao kupunguza machungu ya kushindwa kuwafunga
Oljoro mchezo wa nyumbani wiki iliyopita.
“Simba
sio timu ya kutubabaisha, wanajua soka la Ruvu shooting, mashabiki
wasikose taifa kesho, hakika kutakuwa na burudani kubwa sana, tuko fiti
sana kupambana na mnyama”. Alitamba Masau.
Simba
wanaingia katika mchezo wa kesho wakiwa nafasi ya nne ya msimamo
wakijikusanyia pointi 39 na Ruvu Shooting wanaofundishwa na Charles
Boniface Mkwasa wapo nafasi ya saba wakiwa na pointi 31 kibindoni.
0 comments:
Post a Comment