Na Baraka Mpenja
Wekundu
wa msimbazi Simba leo hii wametoa dozi nyingine kwa maafande wa Mgambo
Shooting kutoka mkoani Pwani baada ya kuwatungua bao 1-0 sifuri katika
mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mchezo
huo uliotawaliwa na soka la ufundi umepigwa katika dimba la taifa
jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa Simba wenye
matumaini makubwana kikosi chao kipya.
Mnyama
sasa amefufua matumaini ya kucheza michuano ya Afrika mwakani, kufuatia
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mgambo leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Katika
mchezo huo, uliochezeshwa na refa Andrew Shamba, aliyesaidiwa na
Abdallah Rashid na Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani, hadi mapumziko,
Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao
hilo lilifungwa na kiungo hatari wa pembeni, Haroun Athumani Chanongo
dakika ya nane, ambaye aliombea mpira katikati ya Uwanja na kuanza
kuwapangua mabeki wa Mgambo kabla ya kumchambua kipa Godson Mmasa.
Ushindi
huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 45, sasa ikizidiwa tatu na Azam
FC inayoshika nafasi ya pili, ambayo Jumapili itamenyana na Mgambo
kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi.
Katika
mchezo wa leo, kocha Mfaransa Patrick Liewig aliwapumzisha wachezaji
kadhaa tegemeo, Mrisho Ngassa, Shomary Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Felix
Sunzu na Mussa Mudde kuelekea mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi,
Yanga Mei 18.
Kikosi
cha Simba SC leo kilikuwa; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’/Omary
Salum, Haruna Shamte, Miraj Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward
Christopher, William Lucian ‘Gallas’/Rashid Ismail, Amri Kiemba,
Ramadhani Singano ‘Messi’/Salim Kinje na Haroun Chanongo.
JKT
Mgambo; Godson Mmasa, Salum Mlima, Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha,
Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja/Mussa Gunda, Peter
Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga na Nassor Gumbo
0 comments:
Post a Comment