Kikosi cha Ruvu Shooting katika moja ya mechi za ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita
Na Baraka Mpenja
Miongoni
mwa klabu zinazotajwa kutandaza soka la kisasa, kucheza kwa ushirikiano
katika idara zote kwa maana ya ngome ya ulinzi, dimba la kati na mhimili
wa kupachika mabao kimiani safu ya ushumbuliaji ni maafande wa jeshi la
kujenga taifa wa mkoani Pwani Ruvu Shooting.
Wakati
makocha mbalimbali wa soka, wachezaji, mashabiki na wadau wakikimwagia
sifa za kumwaga kikosi cha wapiga kwata hao kutoka Pwani, kocha mkuu wa
klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa “Master” ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa
anafurahi sana kupongezwa na wapenzi wa soka kuwa kikosi chake
kimecheza soka safi msimu uliomalizika mei 18 ingawa ameanika madhaifu
ya kikosi hicho kuwa safu ya ushambuliaji haina makali ya kunyoa timu
pinzani.
Mkwasa
alisema mara nyingi wachezaji wake walipata nafasi nyingi sana katika
mechi tofauti, lakini walikuwa wanazichezea sana na kuinyima klabu hiyo
ushindi muhimu ambao ungewafanya washike nafasi nzuri zaidi.
“Kwa
ujumla vijana walicheza vizuri sana ingawa mechi nyingi hatukushinda,
bahati mbaya sana timu imekosa nafasi nzuri, lakini tungekuwa makini
katika nafasi ya ushambuliaji tungefika mbali zaidi msimu uliomalizika
wiki iliyopita”. Alisema Mkwasa.
Kocha huyo
aliongeza kuwa mara zote amekuwa akiwataka wachezaji wake kucheza
kitimu na kuachana na tabia ya kucheza kibinafsi kwani soka hilo
limepitwa na wakati.
“Zamani
kupiga chenga ilikuwa sifa sana, siku hizi soka linachezwa kitimu,
sikatai kutumia uwezo binafsi pale inapobidi, lakini kucheza kitimu
inasaidia timu kufanya vizuri, mimi ni mwalimu, nafundisha soka la
kitimu zaidi, vijanabwamekuwa wakinielewa vizuri sana”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa pia
amewatupia lawama baadhi ya waamuzi waliokuwa wanachezesha mitanange ya
ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2013 kuwa wameboronga sana
hivyo kuwaathiri sana katika michezo yao.
Kocha huyo
aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya wanawake Twigar stars
alishauri waamuzi kujirekebishe sana msimu ujao ili kutojenga mazingira
ya kukosewa imani.
“Kuna
mambo ambayo waamuzi wameyafanya mpaka aibu, kila mtu alikuwa anashangaa
uwanjani kwa kile kinachotokea, lakini waamuzi huwa wana mamlaka
makubwa sana uwanjani, ndio maana tunakaa kimya, binafsi nawaaomba
wabadilke na kamati ya kutathmini waamuzi iliangalia hilo kwa kina”.
Kujiandaa na msimu ujao Mkwasa alisema kuwa lazima aongeze washambuliaji wa kuongeza makali zaidi msimu ujao.
Mkwasa alisema akipata washambuliaji wazuri wa kati na mawinga atakufa na mtu msimu ujao na kuingia tatu bora ni lazima.
Msimu wa
ligi kuu uliomaliza mei 18 mwaka huu, Ruvu shooting walikipiga na Toto
Africans ya Mwanza walioshuka daraja na kuambulia kipigo cha mabao 2-0
na kufikisha pointi 32 katika nafasi ya saba.
Mkwasa alisisitiza kuwa kumaliza nafasi ya saba haijampa faraja hata kidogo kwani hesabu zake zilikuwa kukaa nafasi tatu za juu.
0 comments:
Post a Comment