WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani
ya Simu “MKUU
POLISI”
&
nbsp; Ofisi ya Inspekta Jenerali
wa Polisi,
Simu
: (022) 2110734
Makao Makuu ya Polisi,
Fax
Na. (022)
2135556
S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja: DAR ES SALAAM.
8 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano
wa kumi na nane wa mwaka kwa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za
Kusini mwa Afrika (SARPCCO) unatarajia kufanyika Mei 15, 2013
jijini Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wa umoja huo kwa mwaka
2012/2013 Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania, IGP Said Mwema.
Mkutano
huo utatanguliwa na Mkutano wa kamati tendaji za SARPCCO ambao
utafunguliwa na IGP Said Mwema Mei 13, 2013 na kufuatiwa na Mkutano wa
Wakuu wa Polisi wa nchi hizo utakaofunguliwa Mei 15, 2013 na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt Emmanuel Nchimbi.
Katika
mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi ya kukabiliana
na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za pamoja na
ushirikiano baina ya SARPCCO na Umoja wa Wakuu wa Polisi wa nchi za
Afrika Mashariki (EAPCCO).
Vilevile,
mkutano huo utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa
Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na
kamati tendaji ya Jinsia na watoto katika mkutano wao uliofanyika mwezi
Machi jijini Dar es Salaam.
Aidha suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano huo.
SARPCCO
iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya
uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na nne ambazo
ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Congo,
Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland na
Madagascar.
Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment