Kocha
Mkongwe kuliko wote ligi kuu soka Tanzania bara msimu huu, Abdallah
Kibadeni “King Mputa” (Kulia) saa chache zijazo kuoneshana shughuli na
Mkwasa wa Ruvu Shooting uwanjani Kaitaba mkoani Kagera
Charles Boniface Mkwasa (Kushoto) atauweza utaalamu wa Kibadeni leo Kaitaba?
Na Baraka Mpenja
Leo
hii dimba la kaitaba kanda ya ziwa katika mkoa wa Kagera litahimili
madalagu ya wakata miwa wa Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Ruvu
shooting kutoka mkoani Pwani.
Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao wa MATUKIO DUNIANI
kutoka mkoani Kagera, Afisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema
hali ya hewa ya kaitaba mchana huu ni nzuri na wanamuomba mungu mvua
isinyeshe kwani uwanja huo una mashimo ambayo yanatuamisha maji.
“Kwa
kweli uwanja wa kaitaba una mashimo na kama mvua itanyesha leo hii kabla
ya mechi hakika mambo yatakuwa mabaya”. Alisema Masau.
Akizungumzia
hali ya kikosi chao, Masau alisistiza kuwa mwalimu wa timu hiyo Charles
Boniface Mkwasa “Master” amewapanga vijana wake kupata ushindi mbele ya
Kagera na mpaka sasa hakuna majeruhi hata mmoja.
Kwa
upande wa Kocha wa Kagera sugar, Abdallah Kibadeni “King Mputa” alisema
maandalizi yamekamilika na wamejiandaa kupata ushindi mbele ya Shooting
huku wakiwa na machungu ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0
na Polisi Morogoro.
“Tunamshukuru
Mungu Kagera kwema na hali ya hewa nzuri, leo hii tumejiandaa kushinda
na si vinginevyo, nawaomba mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kubwa”.
Alisema King Mputa.
Ingawa
timu zote mbili hazipambani kutafuta ubingwa ambao tayari umetwaliwa na
Yanga wala kukwepa kushuka daraja, mechi hiyo bado ni muhimu kwao
katika mazingira matatu tofauti.
Kagera
Sugar inayonolewa ikiwa na pointi 40 yenyewe inasaka moja kati ya
nafasi nne za juu ambazo zina zawadi kutoka mdhamini wa ligi, lakini pia
timu zinazoshika nafasi hizo za juu zinapata tiketi ya kucheza michuano
ya BancABC Super 8.
Kwa
upande wa Ruvu Shooting ya Kocha Charles Boniface Mkwasa yenye pointi 31
inasaka moja ya nafasi sita za juu ambazo ni fursa ya kuingia kwenye
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) ambayo inatarajiwa kuundwa baada
ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 28 mwaka huu.
Wagombea
nafasi za uenyekiti na makamu wake ni lazima watoke katika timu
zilizoshika nafasi sita za juu katika VPL msimu uliopita.
Uchaguzi wa TPL Board utafanyika siku moja kabla ya ule wa TFF uliopangwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment