Waziri mkuu mh. Mizengo Pinda amewataka watanzania kuwa watulivu
wakati uchunguzi wa tukio la shambulio la bomu lililotokea katika
kanisa la Mtakatifu Joseph jimbo la Arusha ukiendelea.
Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akitoa taarifa za awali juu ya tukio
hilo bungeni , na kusema suala hilo sio la kushabikia kisiasa badala
yake watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwanasa
waliohusika.
Licha ya watu watatu kupoteza maisha , Waziri mkuu amesema hali ya
majeruhi wa mkasa huo inaendelea vizuri ambapo 24 kati ya 66
wameruhusiwa baada ya kupata nafuu.
Aidha mh. Pinda amesema mpaka hivi sasa , vyombo vya usalama
vinaendelea na uchunguzi iwapo bomu hilo la kurushwa kwa mkono
lilitengenezwa kienyeji au kiwandani.
Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Shamsi Vuai Nahodha ametoa wito kwa wananchi na viongozi wa dini kutoa
ushirikiano kwa kupinga mauaji yanayoendelea hapa nchini.
Mpaka hivi sasa watu wanane wamekamatwa ambapo wanne wana asili ya
kutoka Uarabuni na wengine ni watanzania wakihusishwa na tukio hilo.

0 comments:
Post a Comment