WAZIRI
mkuu Mh. Mizengo Pinda amesema Serikali ina kazi kubwa ya kushughulika
na kundi dogo linalojihusisha na lugha za uchochezi wa kidini ambao
unachangia kudhoofisha amani ya nchi.
“Tunajua nia yao ni kufanya nchi isitawalike lakini sisi tumesema hatukubali. Tumekubaliana na Waziri wa Mambo ya Ndani, ulinzi uimarishwe kila mahali, msishangae kuona watu wanawahoji lakini kwa nia njema, ya kurudisha amani yetu,” Alisema mheshimiwa Pinda.

Mh.
Pinda Ametoa kauli hiyo leo wakati akiwasilisha salamu za rambirambi kwa
niaba ya Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya waumini watatu wa
Kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi,
Parokia ya Olasiti, jijini Arusha waliofariki dunia kutokana na
mlipuko wa mabomu uliotokea Jumapili iliyopita, Mei 5, mwaka huu kanisani hapo.
Waziri Mkuu amewaomba wanachi kutoka ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia kwenye upelelezi wa tukio hilo.
“Ninawaomba Watanzania tushirikiane kuwafichua watu hawa waovu kwa sababu tunaishi nao, ni watu ambao wako miongoni mwetu… Tusaidieni kutunong’oneza ili tuchukue hatua”, . Alisisitiza mh. Pinda.
Waziri Mkuu alisema yeye ni miongoni mwa watu wanaoamini kwamba ukristo au uislamu hauwezi kuondolewa kwa kuwaua viongozi wa dini au waumini wao. “Ni kujidanganya tu mtu akiamini kuwa akimuua Askofu,Mufti au Muumini ataimaliza dini yoyote. Madhehebu haya mawili ni nguzo kubwa kwa Taifa letu, tunatamani tuendelee kuwa na amani iliyokuwepo siku zote,” alisisistiza Mh. Pinda.
Alisema Serikali kupitia idara ya maafa itatoa sh. milioni 100/- ili zisaidie kukabiliana na janga lililowakabili wana Arusha.

Mapema,
akiongoza ibada hiyo, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo aliwataka
waumini wote kutolipa uovu kwa uovu bali watende wema ili kusahihisha
maovu. “Ishara ya uovu imetendwa na hawa watu dhidi ya waumini wenzetu
kwa madhumuni yanayojulikana na wao tu bila kuchokozwa
na hawa marehemu ama wale waliko hospitali (majeruhi),” alisema.
“Uovu umeshatendwa, je sisi tufanye nini? Angekuja hapa kanisani Yule aliyesababisha mauti haya, tungemfanya nini?” Alihoji Kardinali Pengo na kujibiwa na mamia ya waumini waliohudhuria ibada hiyo: “Tungemsamehe.”

Aliwasihi waumini wote kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania ili tukio
hilo na lile la kuuawa kwa Padre Evarist Mushi kule Zanzibar yasiwe
sababu ya kusambaratika kwa amani ya Taifa hili.
“Tusilipe ubaya kwa ubaya, tuendelee kuomba Mungu asikie sala yetu na awazindue wenye mamlaka watimize wajibu wao,” alisema.
Naye
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.
Alex Malasusa akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Jukwaa la
Wakristo Tanzania (TCF), alilaani waliosababisha mauaji hayo na kusema
kitendo hicho kimelitia doa Taifa kwa vile ni kitendo kinachoashiria
kuchafua amani ya Tanzania.
Aliwasihi waumini wote kutokuwa waoga katika kazi ya kumtangaza Kristo.
“Risasi zinapigwa, mioto inayowashwa katika makanisa yetu na mabomu
yanayolipuliwa yasiwe sababu ya kututia hofu. Imani yetu haiku katika
miili bali iko mioyoni mwetu,” alisema.
Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha akitoa shukrani kwa
niaba ya Kanisa Katoliki aliwashukuru wote waliofika kuwafariji
kutokana na tukio hilo na kuwathibitishia kuwa kama Kanisa wameguswa
na moyo waliouonyesha.

Watu
66 waliathirika kutokana na mlipuko huo uliotokea Mei 5, mwaka huu
ambapo watatu wamefariki dunia na kati ya wagonjwa 63 waliobakia, wanane
walihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, wengine waliotibiwa na
kuruhusiwa kurudi nyumbani, na baadhi wanaendelea kupatiwa matibabu
mjini Arusha.
mjini Arusha.
0 comments:
Post a Comment