Na Baraka Mpenja
Maafande
wa Mgambo JKT tayari wameshawasili jijini Dar es salaam “Jiji la Maji
Chumvi” kujiandaa na mchezo wa jumatano ya wiki hii dhidi ya waliokuwa
mabingwa wa msimu uliopita wa ligi hiyo, Mnyama Pori, wekundu wa
Msimbazi Simba utakaotandikwa majira ya saa 10 jioni kwa saa za afrika
mashariki.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo Antony Mgaya ameimbia MATUKIO DUNIANI
kuwa wamewahi ili kuzoea hali ya hewa ya Dar es salaam pamoja na
kufanya mazoezi ya mwisho kuvaana na Mnyama mwenye hasira ya kupoteza
taji lake msimu huu mbele ya wanajangwani, Dar Young Africans.
“Bado
tuna mechi tatu ili kumaliza msimu wa ligi kuu, mojawapo ni hiyo ya
Simba, tunajua fika kuwa Simba ni timu nzuri lakini tuko sawa sawa na
tumejiandaa sana kukabaliniana nao”. Alitamba Mgaya.
Mgaya
aliongeza kuwa kocha mkuu wa maafande hao wa jeshi Mohamed Kampira
anaendelea kurekebisha makosa madogo madogo yaliyopo katika kikosi chake
na kufikia kesho kutwa wanaamini shughuli itakuwa nzuri na simba lazima
wasumbuke.
“Tunamshukuru
maulana wachezaji wote wapo salama na wana morali kubwa sana ,ikumbukwe
hatuko tayari kushuka daraja na tunahitaji pointi zaidi ili kujinusuru,
licha ya Simba kuwa wazuri wanapocheza taifa na hapo jana wameshinda
mabao 3-1 dhidi ya Shooting, sisi tumejiandaa kwa hilo”. Aliongeza
Mgaya.
Akizungumzia
wapinzani wao Simba, Mgaya alisisitiza kuwa Simba wameonekana kuwa na
hesabu nzuri za kuandaa kikosi cha msimu ujao, ndio maana wameanza mbali
kuwaandaa wachezaji wazuri ambao kwa sasa wanacheza soka la kisasa
kuliko mafaza waliozoeleka.
“Kikosi
cha sasa cha Simba ambacho kina wachezaji vijana akiwemo Haruna
Chonongo, Messi na wengine, hakika wapo safi sana nakwambia, tunajipanga
sana kukabiliana na vijana hao wenye damu changa”. Alisisitiza Mgaya.
Simba
nao walishatangaza kulinda heshima yao katika mechi zote zilizosalia na
hapo jana waliendeleza kauli yao baada ya kuibuka na ushindi na kesho
kutwa wanajipanga kuendeleza kauli yao.
0 comments:
Post a Comment