Tuesday, May 7, 2013

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wekundu wa Msimbazi Simba “Mnyama pori” ama “Taifa Kubwa” hapo kesho wanawakaribisha maaafande wa Mgambo Shooting kutoka jijini Tanga katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara dimba la taifa jijini Dar es salaam.
 Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10.30 jioni vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C na B wakati VIP A ni sh. 20,000.
Simba SC inahitaji kushinda mechi hiyo ili kuimarisha mbio zake za kuifukuza Azam FC katika nafasi ya pili.
Mabingwa hao wa msimu uliopita, kwa sasa wana pointi 42 na wanaiombea duwa mbaya  Azam, ipoteze mechi zake mbili zilizobaki na wao washinde mechi zao mbili dhidi ya Mgambo kesho na Yanga SC Mei 18, wawe wa pili.
Simba SC inaweza kufikisha pointi 48, ambazo tayari Azam FC inazo. Ikiwa Azam itapoteza mechi mbili zilizobaki na Simba ikashinda zote, mshindi wa pili ataamuliwa kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.  
Kuelekea katika Mchezo wa Kesho Mgambo JKT kupitia kwa katibu wake Antony Mgaya walisema maandalizi yamekamilika na wanajiandaa kupambana kufa na kupona kutafuta ushindi mbele ya Simba wenye machungu ya kupoteza ubingwa wao.
“Ni mechi ngumu kwetu lakini tumejiandaa kwa uzuri kabisa kutafuta ushindi muhimu mbele ya simba”. Alisema Mgaya.
Nao Simba kupitia kwa kocha msiaidizi, Jamhuri Kiwhelu Julio walisema wao wameshakamilisha kikosi cha kuwafunga wapinzani wao kwani vijana wao wanaonekana kuwa vizuri zaidi.
“Simba ya vijana inaendelea kukaa vizuri, kesho tuko shwari kuibuka na ushindi’. Alisema Julio.
 Wakati huo huo Mechi namba 111 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyochezwa juzi (Mei 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kushinda mabao 3-1 imeingiza sh. 17,700,000.
 Watazamaji 3,163 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,485,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,700,000.
 Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,901 na kuingiza sh. 14,505,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 28 na kuingiza sh. 560,000.
 Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,772,416.50, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,063,449.90, Kamati ya Ligi sh. 1,063,449.90, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 531,724.95, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 206,781.93 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh. 206,781.93.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video