Na Baraka Mpenja
Shangwe,
nderemo na vifijo vimetawala miongoni mwa mashabiki wa kandanda katika
jiji la Tanga baada ya klabu ya maafande wa Mgambo JKT kufanikiwa
kubakia ligi kuu msimu ujao.
Katibu mkuu wa klabu hiyo Antony Mgaya ameimbai MATUKIO DUNIANI kuwa
ushindi wa jana wa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa CCM
Mkwakwani Mkoani Tanga umewapa furaha kubwa baada ya kuumiza vichwa vyao
kwa muda mrefu wakihitaji kutafuta njia ya kubakia ligi kuu.
“Ilikuwa
ngumu sana kwetu, ushindani ulikuwa mkubwa, kuna wakati tukakosa
matumaini baada ya kufungwa kila mchezo muhimu kwetu, lakini tukaendelea
kujipa moyo na hatimaye tumefanikiwa”. Alisema Mgaya.
Mgaya
aliyeonekana kuikubali imani ya dini kuwa Menyezi Mungu amewaona na
kuwasaidia alisema Mungu amesikia kilio chao wakati wa vita ya kukwepa
mkasi wa kushuka daraja .
“Kila mtu
alikuwa anamuomba mungu ili anusurike, lakini katusaidia sisi kwa kutupa
nguvu ya kupambana mpaka mwisho”. Mgaya Alisema kwa furaha kubwa.
Kiongozi
huyo alisisitiza kuwa mafanikio hayo si yao pekee, bali ni ya Mkoa mzima
kwani mashabiki, viongozi na wadau wa soka waliwaunga mkono sana mpaka
mwisho wa ligi.
Mgaya
alisema sasa wamemaliza ligi salama na wanamsubiri kocha wao Mohamed
Kampira aandike ripoti yake itakayojumuisha mapendekezo ya usajili , na
viongozi wapo tayari kuanza shughuli ya kutafuta wachezaji wapya.
“Ulikuwa
msimu wa kwanza kwetu, tumejifunza mengi sana, lazima tusajili wachezaji
wengine ili kuendana na ushindani wa ligi hii msimu unaokuja”. Alisema
Mgaya.
Timu zilizoshuka daraja ni tatu ambazo ni wana kishamapanda Toto Africans, Polisi Morogor na Africa Lyon.
Na timu
mpya ni tatu ambazo ni Mbeya City ya Mbeya, Maafande wa Rhino Rangers
kutoka Tabora na wauza Mitumba wa Ashant United kutoka jijini Dar es
salaam.
Msimu mpya wa ligi kuu unatarajia kuanza kati ya mwizi Agosti na Septemba maka huu.
0 comments:
Post a Comment