Na Baraka Mpenja
Nahodha
na mlinzi wa kushoto wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania “Taifa
stars” na sasa kocha mkuu wa klabu ya soka ya Mtibwa sugar “wana TamTam”
na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mecky Mexeme amekiri kuwa msimu
huu wa ligi kuu soka Tanzania bara umekuwa mgumu zaidi kutokana na uwezo
mkubwa wa kila timu shiriki.
Mexime ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa unaweza kujipanga kupata ushindi katika mchezo fulani lakini ukapata matokeo mabaya tofauti na matarajia yako.
“Binafsi
naamini ligi yetu inazidi kuwa ngumu kadri miaka inavyozidi kwenda,
msimu huu timu zimejipanga sana licha ya kuwepo kwa changamoto
mbalimbali za kifedha na kiutawala, kama misimu inayokuja itakuwa hivi
hakika kupata nafasi tatu za juu itakuwa shughuli pevu”. Alisema Mexeme.
Kocha
huyo mwenye historia ya kuzikataa timu za Simba na Yanga wakati wake wa
soka na kujikita na wakata miwa wa mashamba ya miwa ya Manungu Turiani
aliongeza kuwa kikosi chake msimu huu kimechanganya damu changa na
wakongwe.
“Vijana
wangu wanacheza vizuri na kuleta matumaini ya kufanya makubwa siku za
usoni, wakongwe pia wanaonesha kiwango kikubwa hivyo naweza kusema kuwa
wachezaji wote wanacheza vizuri sana”. Alisisitiza Mexme.
Mexime
mwenye sifa ya uzalendo aliongeza kuwa kwa sasa hesabu zake ni kushinda
mchezo wa funga pazia la ligi kuu msimu wa 2012/2013 dhidi ya maafande
wa Jeshi la Kujenga taifa kutoka mkoani Pwani JKT Ruvu mei 18 mwaka huu
uwanja wa Chamazi uliopo Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
“Nafikiri
mechi ya mwisho ni muhimu sana, natarajia kuibuka na ushindi kutokana
na maandalizi mazuri ninayofanya hapa Manungu, baada ya hapo nitakaa
chini na kuandika ripoti yangu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi”. Alisema
Mexme.
Mchezo
uliopita kocha huyo aliiongoza Mtibwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi
ya vibonde wa ligi hiyo Africa Lyon ambao kwa sasa wanaweza kutoa mkono
wa bai bai kucheza ligi hiyo na kuanda zao ligi daraja la kwanza.
Mabao
yote katika mchezo huo yalifungwa na nyota wao anayekodolewa macho na
baadhi ya timu vigogo ili kuinasa saini yake msimu ujao, Hessein Javu.
Uwezo
wa kufumania nyavu wa Nyota huyo, nidhamu ya mzaoezi na umakini wa
kucheza na nafasi ndio siri kubwa ya kupata mfanikiao klabuni hapo.
Mtibwa
Sugar kwa sasa wapo nafasi ya sita wakiwa na pointi 39 sawa na Simba
lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa
0 comments:
Post a Comment