Monday, May 20, 2013

Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu (Picha kwa hisani ya Fununublog)
……………………………………………
Watuhumiwa  70  wa vurugu  za machinga  na polisi mjini Iringa akiwemo mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Peter  Msigwa   wamefanyiwa  utaratibu  wa  dhamana  kutokana na mahakama  kukubali  kutoa  dhamana  baada ya  kusomewa mashitaka matatu  huku mbunge  akisomewa mashitaka mawili likiwemo  kushawishi  na kufanya mkutano bila  kibali  .

Watuhumiwa  wote  wamekana  mashitaka  dhidi walikuwa wakifanyiwa  utaratibu  wa dhamana  katika  mahakama  hiyo ya  hakimu mkazi  wa wilaya ya  Iringa Mheshimiwa  Godfrey Isaya .

Hata  hivyo wamekana  mashitaka  yote yaliyotolewa ambayo shitaka la kwanza la mbunge ni kushawishi kufanya vurugu  ,huku  wengine  wote  kosa la kwanza kufanya mkutano bila kibali , kuharibu mali kinyume na sheria na  kufanya  vurugu .
Dhamana ya watuhumiwa hao ilikuwa ni wadhamini wao  kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 1 na  kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama
Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo
Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video