Na Baraka Mpenja
Mabingwa
wapya wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Yanga ya Dar es salaam “Wazee
wa Uturuki” wanaendelea kuimarisha mawindo yao juu ya watani zao wa jadi
waliovuliwa taji msimu huu, wekundu wa Msimbazi Simba “Taifa kubwa”
utakaopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam mei 18 mwaka huu.
Afisa habari wa klabu ya Yanga, Baraka Kizuguto ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa
wachezaji wanaisubiri kwa hamu mechi hiyo ambayo ni maalumu kwao
kunogesha ubingwa wao walioutwaa msimu huu kwani wasiposhinda mechi hiyo
taji lao litaingia shubiri.
“Tunaendelea
vizuri na mazoezi, wachezaji wote wapo salama na tunahitaji ushindi
katika mchezo wetu wa mwisho ambao tutapambana na watani wa jadi Simba
ambao mechi za mwisho wanakuja vizuri, lakini tunaimarisha mawindo
yetu”. Alisema Kizuguto.
Kizuto alisisitiza kuwa Yanga wamejipanga sana msimu huu na kuwazuia katika mchezo wowote ule ni kazi ngumu sana.
Afsia
habari huyo alisema wachezaji wa Yanga “Watoto wa Jangwani na Twiga”
wamekuwa wakiambiwa kuwa raha ya ubingwa ni kumpiga mtani wako, hivyo
maandalizi ni mazuri na lazima washinde mechi hiyo ya mwisho.
“Kila
mchezaji wetu anajua wajibu wake, Simba ni timu nzuri na vijana wao
wanacheza kwa uzuri, lakini sisi tunajipanga barabara”. Alisema
Kizuguto.
Pia
alisema Yanga inayoongozwa na wachezaji nyota kama Haruna Hakizimana
Fadhil Niyonzima, Khamis Kiiza, Frank Domayo, Simon Msuva na wengine
wengi itacheza soka safi na la kuvutia mbele ya maelfu ya mashabiki wa
klabu hizo.
Wakati
Yanga wakijiwinda na mechi hiyo, Simba waliopo nafasi ya tatu
wakijikusanyia pointi 42 kibondoni baada ya kushinda mchezo wa jana
dhidi ya Ruvu Shooting mabao 3-1 uwanja wa taifa, wao wamebakiza mechi
mbili ambapo kesho kutwa jumatano watashuka dimbani kuvaana na maafande
wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga.
Kwa
mujibu wa kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kiwhelu “Julio Alberto”,
alisema kwa sasa timu inaandaliwa kwa ajili ya mchezo wa kesho kutwa na
baada ya hapo watahamishia akili zao katika mchezo wa watani wa jadi mei
18 mwaka huu.
“Kila
mtu anaona maendeleo ya timu, vijana wanaimarika kila mechi, nadhani
mechi dhidi ya Yanga tutawafunga na kubakisha heshima yetu pale pale”.
Alisema Julio.
0 comments:
Post a Comment