Na Baraka Mpenja
Mwaka huu imeishia raundi ya tatu ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Ilianza
kwa kuwafunga Al Nasri Juba ya Sudani kusini mabao 3-1 uwanja wa taifa,
ikamalizia kazi Sudan kwa kushusha dhahama ya mabao 5-0. Ikaelekea
Liberia na kukutana na Barrack YC ya huko, wakaindatika 2-1 nyumbani
kwao na waliberia walipotia maguu yao Dar es salaam wakajikakamua na
kulazimisha suluhu ya bila kufungana.
Safari yao
ikaendelea kwa kukutana na AS FAR Rabat ya Morroco uwanja wa taifa,
mchezo wa kwanza walilazimishwa suluhu pacha ya bila kufungana, baadaye
wakakwea pipa na kuelekea Morroco ambapo wakafungwa 2-1 huku Bocco
akikosa mkwaju wa penati dakika ya 83 na kama angetia kambani wangesonga
mbele hatua ya makundi.
Baada ya
hapo Azam fc wana lambalamba walirejea nyumbani na Kuahidi kutafuta tena
nafasi ya kucheza michuano hiyo mwakani ambapo tiketi pekee ni kushika
nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Leo hii
katika uwanja wao wa nyumbani Chamazi, Azam fc wameshuka dimbani kuvaana
na maafande wa Mgambo Shooting kutoka mkoani Tanga “Waja leo waondoka
leo” huku wakihitaji sare ama suluhu ili kupata pointi moja na
kujihakikishia nafasi ya pili msimu huu.
Hatimaye
dakika tisini zilimalizika kwa wachezaji John Bocco “Adebayor” aliyejuta
na kuwaomba radhi watanzania kwa kukosa penati muhimu nchini Morroco,
Kipre Herman Tchetche pamoja na Attudo kufunga bao moja moja na
kurudisha furaha kubwa kwa mashabiki, viongozi na benchi la ufundi la
klabu hiyo chini ya kocha Muingereza Sterwat John Hall.
Sasa Azam
wametetea nafasi yao ya umakamu bingwa baada ya kufikisha pointi 51 na
kuwachinjilia mbali wekundu wa Msimbazi Simba waliokuwa wanawania nafasi
hiyo.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI
dakika chache baada ya kipute hicho kumalizika katika dimba la Chamazi,
Afisa habari wa klabu ya Azam fc Jafar Idd Maganga amesema ushindi wa
leo umetokana na mipango waliyojiwekea tangu wapoteze mchezo nchini
Morroco.
Jafar
alisema baada ya kutolewa na FAR Rabat walisikitika sana na wakajipanga
kurejea tena katika mashindano hayo mwakani na mipango yao ilikuwa
kushidna mchezo wa leo ili kuitwaa nafasi ya pili na kuiwakilisha nchi
kwa mara nyingine michuano ya kimataifa na hatimaye wameweza leo hii.
“Azam
imedhihirisha kuwa ni timu nzuri na inacheza soka safi, tutaendelea
kuwapa burudani mashabiki wetu na sasa tunajipanga zaidi kufanya vizuri
michuano ya kimataifa zaidi ya mwaka huu”. Alisema Jafar.
Jafar
aliongeza kuwa baada ya ushindi wa leo wataendelea kukaa kambini
kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya maafande wa JKT Oljoro katika
dimba la Shekh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha.
Azam fc
msimu wa mwaka jana walikuwa katika kinyang`anyiro cha kuwania ubingwa
na Simba, mwaka huu Simba kajitoa na kuwaacha wana lambalamba hao kubaki
na wanajangwani katika mbio za kuwania ubingwa, lakini mbio hizo
zimeishia ukingoni kwa Yanga kutwaa taji msimu huu na kupata nafasi ya
kucheza ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
0 comments:
Post a Comment