Intermillan
Rais wa klabu ya Intermillan Massimo Moratti leo kupitia
vyombo mbalimbali vya habari amedokeaa kuwa aliyekuwa kocha wa klabu ya
Manchester City Robeto Macini huenda
akachukua nafasi ya kocha mkuu wa klabu
hiyo, Andrea Stramaccion mwishoni mwa
msimu huu
Pichani, rais wa klabu ya Intermillan, Massimo Moratti |
Lakini
Moratti alipoulizwa kama Macini ni
chaguo sahihi kwa klabu yake, alisema kwaa
upande wake anaamini ni chaguo sahihi, huku akisisitiza kuwa maamuzi ya mwisho wa kandarasi wa klabu hiyo
kwa sasa Andrea Stramaccion bado hayajafikiwa rasmi.
Manchester united.
Baada ya nyota wa soka wa klabu ya
Manchester United , Wayne Rooney, kutangaza nia ya kuihama klabu hiyo mwishoni
mwa msimu huu, klabu ya Chelsea pamoja nao Bayern Munich wametangaza nia ya kumsahinisha
nguli huyo.
Wayne Rooney. |
Rooney ambaye amefanikiwa kuchukuwa vikombe vya ligi kuu nchini Uingereza mara tano tangu ajiunge na klabu ya mashetani
wekundu amesema licha ya kuwepo kwa tetesi hizo kutoka Chelsea na Bayern
Munich, yeye anavutiwa zaidi zaidi na
klabu ya PSG kwani anahisi huko ndiko wanaweza kumlipa vizuri lakini anafurahia
kuungana na mshambuliaji wa klabu hiyo Zlatan Ibrahimovic.
EXLUSIVE:
Pichani hapo juu ni Rooney akiwa kwenye pozi na familia yake. |
Mzee
mzima Rooney amefanikiwa kumpata mtoto mwingine wa kiume juzi
Jumatatu May 20, 2013 na kufikisha idadi ya watu wannne katika familia
hiyo.
Aidha
mke wake Rooney, Coleen Rooney amesema binafsi anamshukuru Mungu kwa
kumpa mtoto mwingine wa kiume 'Klay' na kufanya idadi ya watoto wao
kufikia wawili. Mtoto wa kwanza wa Rooney anaitwa Kai, alizaliwa mwaka
2009
Mchezaji wa
zamani wa kati wa klabu ya Borussia Dortumund Steffen Freund amesema baada ya klabu ya Bayern Munich kutolewa kwenye fainali ya klabu bingwa barani Ulaya na klabu ya Chelsea
mwaka jana, kwa sasa anaamini klabu hiyo ina usongo mkubwa kueleke fainali ya
klabu bingwa ulaya dhidi Borussia Dortumund itakayochezwa jumamosi hii dimbani
WEMBLEY.
Baadhi ya wachezaji Bayern Munich wakisikitika baada ya kupoteza UEFA dhidi ya Chelsea 2011/2012. |
Steffen Freund ambaye pia kwa sasa ni kocha msaidizi katika klabu ya Tottenham
amesistiza kuwa licha ya Bayern
kupewa kipaumbele katka fainali hiyo, Borussia Dortmund nao siyo wa kubezwa
kwani kwa sasa wamekuwa katika hali nzuri toka hatua ya makundi ya michuano
hiyo.
0 comments:
Post a Comment