Na Baraka Mpenja
Michuano
ya vijana kwa umri wa miaka chini ya 12 (under 12) na 14 (under 14)
inayosimamiwa na chama cha soka la vijana wilaya ya Ilala (IDYOSA)
inatarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo kesho (mei 4) katika dimba la
kumbukumbu ya Karume Ilala jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa IDYOSA Faza Edwirn Mloka ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa
maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda kufika ili
mashabiki wa kandanda washuhudie vipaji vipya kwa vijana ambao
watalibeba taifa siku za usoni.
“Michuano
imeandaliwa kwa uzuri sana na matumaini yetu ni ushindani mkubwa kwa
timu shiriki huku kanuni na sheria 17 za mchezo wa soka zikitumiwa”.
Alisema Mloka.
Mloka aliongeza kuwa tayari waamuzi wameshapangwa tayari kwa kuanza kwa mitanange hiyo ya mayoso.
“Kwa
sasa soka la vijana ndio msingi wa taifa lolote lile duniani,
tumeshazalisha vijana wazuri kama Abubakar Salmu “Sure Boy” na Frank
Domayo, hakika ni mavuno ya michuano hii, wadau wajitokeza kwa wingi
kushuhudia vijana wadogo wakifanya vizuri”. Alisisitiza Mloka.
Kwa
upande wake katibu mkuu msaidizi wa IDYOSA Saidi Pamballelo alisema kwa
mwaka huu timu zote zimejipanga vizuri kutokana na kupata muda mrefu wa
maandalizi.
Pia Pamballelo ametaja ratiba ya kesho na kesho kutwa kama ifuatavyo;
Tarehe 4/05/2013.
1.stone city (vs) new team
2.makoba (vs) home team
3.kulasini orphans center (vs) bom bom
4.vumbua vipaji ( vs) real boys
Ratiba ya tarehe 5/may/2013 siku ya jumapili
1.toto f.c (vs) e elimu .f.c
2.amana shooting( vs) barcerona
3.kinota f.c (vs) nuru .f.c
4.kinota (vs) tabata rangers
Aidha
Pamballelo aliongeza kuwa wao wamejipanga vizuri na kuzingatia sheria
zote na mwaka huu hakuna vijeba kwani timu zote zilifanyiwa usaili
makini sana.
0 comments:
Post a Comment