Pellegrini anatajwa kama mmoja wa walimu
wenye nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake mwishoni mwa msimu na
Mancini anatarajia kupewa ufafanuzi kutka kwa mabosi wa City baada ya
Mkurugenzi wa Soka, Txiki Begiristain kukutana na mwakilishi wa kocha
huyo wa Malaga kwa chakula cha jioni mjini Madrid.
Alipoulizwa kama Mwenyekiti, Khaldoon Al
Mubarak alimuambia kama atabaki kazini, kocha huyo wa City alisema:
"Hajawahi, hajawahi. Hatuna haja ya kulizungumzia hili. Hatuna matatizo
yoyote. Tuna uhusiano mzuri. Katika miaka miwili, tumeshinda mataji
matatu, na sasa tuna nafasi ya kushinda taji lingine moja,"alisema.
Katikati ya lolote: Roberto Mancini amesema mustakabali wake upo kizani Manchester City
Wa pili bora: Manchester City imeshindwa kutetea taji la Ligi Kuu msimu huu
'Ikiwa katika miaka mitatu nisingeshinda
taji, hapo sawa, lakini tumefanya kazi nzuri hadi sasa. Tuna nafasi ya
kutwaa Kombe la FA na kuwa wa pili katika msimamo wa Ligi Kuu. Baada ya
hapo, Mwenyekiti anaweza kuchukua uamuzi wowote kuhusu kocha, Hatuna
tatizo lolote. Nimechanganyikiwa, kwa sababu nataka kushinda taji la
pili la Ligi Kuu. Tulikuwa na nafasi, lakini wakati mwingine unaweza
kufanya makosa.
"Unaweza kumuuliza maswali hayo Txiki, lakini si muhimu kwangu. Nafikiri alikuwa ana chakula kizuri cha jioni.
Majadiliano: Txiki Begiristain (kulia) alifanya mazungumzo na wakala wa Manuel Pellegrini wakati wa chakula cha jioni
Anatakiwa: Kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho amekuwa akihusishwa pia na kuhamia Etihad
"Kwa miezi sita iliyopita, watu
wameandika kila kitu, walianza na Pep Guardiola na Jose Mourinho, kisha
Pellegrini, Carlo Ancelotti na Brendan Rodgers. Najua nafanya kazi na
watu makini, kama Khaldoon na Sheikh Mansour, lakini kama kulikuwa kuna
kocha mwingine aliyeshinda mataji matatu ndani ya miaka miwili,
usingesema kitu juu yake."
Mancini tayari ameanza mikakati ya msimu
ujao na angependa kuongeza mshambuliaji, beki wa kati, kiungo mkabaji,
mchezeshaji na winga.
Lakini kutokana na kuingia kwenye uhusiano mbaya na baadhi ya wachezaji waandamizi mustakabali wake uko kwenye hatihati.
0 comments:
Post a Comment