Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Spormail.com, Soka In Bongo
WAMEPOKONYWA
TAJI lao la Ubingwa wa England na Manchester United, wametupwa nje
hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na sasa wamebakisha FA CUP tu
kuokoa Msimu wao, na pengine kumnusuru Meneja wao Roberto Mancini,
Manchester City leo hii majira ya saa moja na robo usiku wanacheza
fainali ya kombe la FA dhidi ya Wigan Athletic, Timu ambayo ipo hati
hati kushushwa Daraja.
Hii ni Fainali ya 10 kwa Man City kwenye FA CUP na kwa Wigan ni Fainali ya kwanza tangu Timu yao ianzishwe Mwaka 1932.
Kwa
Man City, hii ni Mechi rahisi hasa kwa kukutana na Wigan Athletic ambayo
kwenye Ligi, BPL,Barclays Premier League, ipo hatarini kushusuhwa
Daraja.
Manchester
City wanatinga Fainali ya FA CUP kwa mara ya 10 tangu kuundwa kwa Timu
yao na wametwaa Kombe hili mara 5 katka Miaka ya 1904, 1934, 1956, 1969
na 2011.
Pia, Man United wameshatokea Washindi wa Pili mara 4 katika Kombe hili Miaka ya 1926, 1933, 1955 na 1981.
Man City wakiwa ndio wamechaguliwa kuwa ‘wenyeji’ kwenye Fainali hii, Wigan watalazikimika kuvaa Jezi zao za ugenini Nyeusi.
Hii itakuwa ni Fainali ya 132 ya FA CUP na ya pili kudhaminiwa na Budweiser, Kampuni ya Bia.
Mshindi
wa Mechi hii hucheza EUROPA LIGI kwa Msimu unaofuata lakini kwa vile
Man City wameshafuzu UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, kwa kutwaa nafasi ya Pili
nyuma ya Mabingwa Manchester United kwenye BPL, Barclays Premier
League, Wigan ndio watatwaa nafasi hii ya kucheza EUROPA LIGI
Wikiendi
bab kubwa: Kocha Manchester City Roberto Mancini akiwa katika kituo
cha Traini jana walipokuwa wanaelekea jijini London
Kitaeleweka leo: mashabiki hawa wa City wapo tayari kupiga “nduru” mwanzo wa mchezo hadi mwisho.
Wachezaji wa Manchester City kama walivyonaswa na kamera ya sportsmail.com katika kituo cha Traini jana.
0 comments:
Post a Comment