Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifurahia kazi za mikono zinazofanywa na
watoto wenye ugonjwa wa akili (autism) wakati alipotembelea Kuwait
Autism Center huko nchini Kuwait tarehe 6.5.2013. Mama Salma amefuatana
na Rais Kikwete katika ziara ya siku tatu ya kiserikali nchini humo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za useremala zinazofanywa na
watu wenye ugonjwa wa akili wa watoto (autism) wakati alipotembelea
Kuwait Autism center tarehe 6.5.2013. Mama Salma yupo nchini Kuwait
akifuatana na Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali ya siku tatu
nchini humo.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,
akifurahia jambo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kuwait Center for
Autism Dr. Samira Al Saad mara baada ya bkusaini kitabu cha wageni baada
ya kuwasiri kituoni hapo tarehe 6.5.2013.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,
akifurahia jambo na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kuwait Center for
Autism Dr. Samira Al Saad mara baada ya bkusaini kitabu cha wageni baada
ya kuwasiri kituoni hapo tarehe 6.5.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa
Kuwait Autism Center Dr. Samira Al Saad mara baada ya kutembelea taasisi
hiyo iliyopo nchini Kuwait tarehe 6.5.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mwanzilishi na Mwenyekiti
wa Kharafi Kids Activity Center Bibi Sabeeka Al Jaser wakati Mama Salma
alipotembelea kituo hicho kilichoko katika jiji la Kuwait tarehe
6.5.2013 kinachotunza watoto na watu wenye matatizo mbalimbali kama vile
wenye mtindio wa ubongo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za uchoraji zinazofanywa na
watu wenye ulemavu wa ubongo wanaolelewa katika kituo Kharafi Kids
Activity Center wakati Mama Salma alipotembelea kituoni hapo tarehe
6.5.2013.
Mama
Salma Kikwete akiangalia ufinyanzi wa vitu mbalimbali unaofanywa na
watu wenye ulemavu kwenye Kituo cha Kharafi huko nchini Kuwait.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na
wafanyakazi wa Kharafi Kids Activity Center baada yan kutembelea kituo
hicho kilichoko katika jiji la Kuwait tarehe 6.5.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana rasmi na Mwanzilishi na Mwenyekiti
wa Kharafi Kids Activity Center Bibi Sabeeka Al Jaser mara baada ya
kutembelea kituo hicho kilichoko Kuwait City tarehe 6.5.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Post a Comment