Na Anna Nkinda – Kuwait
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete amekiomba kituo cha watoto wenye mtindio wa
Ubongo kilichopo nchini Kuwait kushirikina na Tanzania ili waweze
kufanya kazi kwa pamoja ya kuwasaidia na kutoa mafunzo kwa watoto wenye
matatizo kama hayo waliopo nchini.
Mama
Kikwete alilitoa ombi hilo jana alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya
kuona jinsi wanavyotoa mafunzo kwa watoto hao ambayo yameweza
kuwabadilisha akili zao na kuwa sawa na za watu wengine.
Alisema
kuwa watoto wenye mtindio wa ubongo hata nchini wapo na wanapata
mafunzo katika vituo vichache zilivyopo lakini kama watashirikiana kwa
pamoja wataweza kubadilishana ujuzi ambao utawasaidia kutoa mafunzo
mazuri zaidi kwa watoto hao.
“Ninawapongeza
kwa kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya kutoa mafunzo kwa watoto
hawa kwani ni jambo jema kuwasaidia watu wenye matatizo.
“Watoto
hawa wakipewa mafunzo akili yao itakuwa sawa na watu wengine, wakiwa
wakubwa na kufikia umri wa kujitegemea wataweza kufanya kazi mbalimbali
za maendeleo ambazo zitawaingizia kipato na kuwasaidia katika maisha
yao ya baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kituo hicho Dk. Samira Al-Saad alisema kuwa
kama watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo watapelekwa shule
mapema zinazotoa mafunzo kwa ajili yao watapona na kuwa na akili sawa
na watu wengine.
Dk.
Samira alisema kuwa wazazi wengi hawajui kwamba matatizo ya mtindio wa
ubongo yanatibika kama mtoto akipewa elimu ya darasani na kufanyishwa
mazoezi ambayo yatamsaidia kufanya shughuli zake mwenyewe bila ya
kutegemea msaada wa jamaa zao.
“Kituo
hiki kilifunguliwa mwaka 1994 na hadi sasa kina wanafunzi 120 ambao
wanapata mafunzo ya nadharia na vitendo na kinajiendesha kwa kupata
msaada kutoa Serikalini, watu na mashirika binafsi ya ndani na nje ya
nchi”, alisema Dk. Samira.
Aliendelea
kusema kuwa umri wa watoto wa kuanza masomo ni miaka sita hadi 15 na
kama mwanafunzi atakuwa amevuka miaka 15 atajifunza zaidi mafunzo ya
vitendo ambayo yatamuwezesha kujitegemea hapo baadaye.
Dk.
Samira alisema, “Wanafunzi wetu wameweza kupata ajira sehemu mbalimbali
hii ni baada ya kupata mafunzo ambayo yamewafanya kuwa na akili sawa na
watu wengine ambao hawana matatizo haya, kuna baadhi yao tumewaajiri
hapa na hivi sasa wanawafundisha wanafunzi wenzao.
Mama
Kikwete pia alitembelea Kituo cha Al-Kharafi ambacho kinatoa huduma ya
mazoezi kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubungo na kuona jinsi
watoto hao wanavyofanya mazoezi yao.
Kituo
hicho kinapokea watoto wenye umri wa kuanzia miaka minne hadi 12
ambao wanafanya mazoezi kwa kucheza michezo mbalimbali ambayo
inawabadilisha akili zao na kuwa katika hali ya kawaida .
Akiwa
katika kituo hicho alijionea kazi mbalimbali zinazofanywa na watoto hao
ambazo ni uchoraji, ushonaji, upishi pia aliona michezo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na nyimbo na maonyesho ya mavazi.
Mama Kikwete aliambatana na Mumewe Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Kuwait kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
0 comments:
Post a Comment