Na Baraka Mpenja
Uchaguzi
wa viongozi wa klabu ya Maji Maji ya Songea mkoani Ruvuma “Wanalizombe”
umesogezwa mbele hadi mei 31 mwaka huu ili kuwapa nafasi wadau wengi
kujitokeza kuomba nafasi saba zitakazowaniwa katika kinyang`anyiro
hicho.
Awali
mchakato wa uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika kati ya mei 15-20 mwaka
huu lakini sasa utafanyika rasmi tarehe tajwa hapo juu.
Meneja wa klabu hiyo Godfrey Ambrose Mvula maarufu kwa jina la Makete ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa
wanawaomba radhi wadau kwa kusogeza mbele uchaguzi huo lakini kila kitu
kipo sawa na wajiandae kwa tarehe mpya iliyotangazwa.
“Watu
walishajua tarehe mapema, tumeamua kusogeza mbele kwa maslahi ya timu,
tunaamini muda tulioongeza utatumiwa vizuri na wanachama wetu kuomba
nafasi zilizotangazwa”. Alisema Mvula.
Mvula alizitaja nafasi zitakazowaniwa kuwa ni mwenyekiti na makamu wake, pamoja na wajumbe watano wa bodi.
Meneja
huyo alisisitiza kuwa kwa wale wote wenye nia ya kuwarejesha
wanalizombe soka la ushindani ni nafasi kwao kujitokeza ili kufanikisha
azima yao.
“Zamani
ukisikia Maji Maji unasisimka nywele, sasa wakati wa kurudisha ngoma ya
Lizombe umefika na lazima turudi ligi kuu msimu wa 2014/2015”. Alisema
Mvula.
Mvula
aliongeza kuwa baada ya kufanyika uchaguzi huo, viongozi wapya kwa
kushirikiana na wanachama na wadau wa soka mkoani Ruvuma wataandaa
tamasha la “Maji Maji Day” ili kuichangia timu hiyo na kubadilishana
mawazo jinsi ya kuirudisha timu hiyo ligi kuu.
“Tutakuwa
na tamasha kubwa sana, tutawaalika wachezaji wa zamani wa klabu yetu
pamoja na wasanii wa muziki wenye asili ya mkoa wa Ruvuma akiwemo Joseph
Haule “Profesa J” mzee wa Mitulinga.
0 comments:
Post a Comment