Madiwani wakimsikiliza mwenyeki wa Halmashauri Mwenyekiti
wa Halmashauri ya mji mpanda akitoa maamuzi ya kikao cha madiwani
kwenye ukumbi wa chuo kikuu huria cha kumwazimia Mkurugenzi wao Picha
zote na ((Kibada Kibada Katavi.)
Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi.
Sakata
la halmashauri ya mji wa mpanda lililokuwa likiigubika Halmashauri hiyo
kwa muda mrefu la kumkataa Mkurugenzi wa Mji wa Mpanda Joseph Mchina
limeingia katika hatua nyingine kufuatia madiwani wa Halmashauri hiyo
kuitisha kikao cha baraza maalumu la madiwani la kuiomba Serilali
kumuhamisha mkurugenzi huyo kutokana na tuhuma mbalimbali
zinazomkabili.
Akizungumza
katika kikao hicho Mwenyekit Halmashauri ya mji wa Mpanda Enock
Gwambasa alisema baraza hili liligeuka na kuwa kamati maalum kwa ajili
ya kujadili tuhuma mbalimbali zinazowakabili watumishi kwa kufuata
taratibu kanuni na sheria za kiutumishi na kufikia maamuzi ambapo
waliomba serikali kumhamisha mkurugenzi wa mji haraka iwezekanavyo
kufuatia baraza hilo la madiwani kumkataa kutokana na na tuhuma
mbalimbali zinazomkabiri zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha na
mali za Halmashauri iliyosababishia kuipatia hati yenye mashaka kwa
kipindi cha miaka miwili mfululizo.
Tamko
hilo la baraza la madiwani lilitolewa jana kwenye kikao chao
kilicho fanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria Tawi la
Mkoa wa Katavi na kuhudhuriwa na watalaam pamoja na wageni waalikwa.
Baraza
hilo Maalumu la Madiwani lilifanyika kufuatia maamuzi yaliyo
pitishwa na Baraza la Madiwani yaliyotolewa kwenye kikao cha Aprili
4 mwaka huu ambacho kilipanga kuitishwa kwa kikao maalum ndani ya
siku 21 ili kumjadili Mkurugenzi kutokana na tuhuma saba zilizo
kuwa zikimbabili
Katika
Kikao hicho kilianza kwa Mwenyekiti wa Halmashauri YA Mji wa Mpanda
Enock Gwambasa kuwaeleza wajumbe wa baraza kuwa kikao kilikuwa
kifanyika siku moja kabla yaani April 29, lakini Katibu Tawala wa
Mkoa Mhandisi Emanuel Kalobelo aliwaandikia barua ya kusitishwa kwa
kikao hicho kwa kile kilichoelezwa kukiukwa kwa kwa utaratibu wa
kikao namna ya kuitisha Maraza Maalumu la Madiwani la kumjadili
Mkurugenzi wao.
Mwenyekiti
Gwambasa aliendelea kueleza kuwa hata hivyo baada ya mjadala mrefu
baina ya Katibu Tawala na Madiwani walikubaliana kikao kifanyike
siku iliyofuata yaan April 30 kwa kufuata kakuni,taratibu sheria na
miongozo zinavyoelekeza.
Kikao
cha kamati ya Madiwani kilichukua mwendo wa saa 3 kusikiliza na
kujadili tuhuma na kisha madiwani walikaa tena kama Baraza na
kutowa tamko lao lilitolewa na Mwenyeki wa Halmashauri Enock Gwambasa
kwa niaba ya madiwani
Mwenyekiti
alieleza kuwa Baraza limefikia uamuzi wa kuiomba Serikali imuhamishe
kwa kumpangia kituo kingine cha kazi Mkurugenzi Joseph Mchina kwa
kuwa wao madiwani hawamtaji katika Halmashauri yao.
Akifafanua
zaidi Gwambasa lisema maamuzi ya kikao hicho watapelekwa ngazi
husika za juu ili ziweze kufuatilia tatizo la Mkurugenzi huyo na
kuchukua hatua kwa kufuata taratibu za kiutumishi.
Alizitaja
miongoni mwa tuhuma anazotuhumiwa nazo Mkurugenzi Mchina kuwa ni
matumizi mabaya ya fedha za Halmashauri hali iliyosababisha Halmashauri
kupata hati yenye mashaka miaka miwili mfululizo,pia wamekuwa wakitoa
maelekezo lakini hayatekelezwi.
Kwa
upande wake Joseph Mchina alipoulizwa ameupokeaje uamuzi huo habari
wa baraza la madiwani alisema kwa kuwa mambo haya yanakwenda kwenye
ngazi za juu za Serikali ni vyema kusubiri Serikali itatowa maamuzi
gani kwani mapema mno kuzungumzia.
Mbunge
wa jimbo la Mpanda Mjini Said Arfi akizungumzia uamuzi wa uliochukua
na baraza la madiwani nayeye akiwa sehemu ya madiwani kwa mjibu wa
sheria kwa kuwa ni Mbunge wa jimbo la mpanda Mjini alieleza kuwa ni
sahihi na wao wameongozwa na kanuni zao .
Wao
wamependekeza Mkurugenzi ahamishwe kwa kuwa amekaa kwenye kituo hicho
kwa muda mrefu hivyo amekuwa akifanya kazi kwa mazoezi amekaa mpanda
tangu mwaka 2003 alipokuwa Afisa Utumishi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
hadi Mkurugenzi hivyo ni vyema akabailisha kituo cha kazi hapo hata
utendaji katika halimashauri utabadilika kwa kuwa kuna mazoea ya muda
mrefu.
Pia
akashauri zana ya kutelemsha madaraka kwa wananchi kuwa ni muhimu kwa
bado sehemu hiyo hajapatiwa umuhimu madiwani wakawa na maamuzi yao
yakiwa na nguvu kuliko hadi kusubiri maamuzi kutoka juu.hivyo moja ya
mapendekezo waliyoyatoa katika kikao ni vyema wakamhamisha kutoka kituo
kimoja hadi kingine ili kubadilisha utendaji kazi.
0 comments:
Post a Comment