Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kwa niaba ya Rais wa
Zanzibar Dr. Ali Mohammed Sheni akihutubia katika kilele cha sherehe za
mei mosi
Mwakilishi wa shirila la bandari Zanzibar baada ya shirika hilo kuteuliwa kuwa shirika bora katika mashirika ya umma mwaka huu.
Mwakilishi wa Hospilai ya Al Rahma
akipokea zawadi baada ya kuchaguliwa kuwa taasisi binafsi kwenye
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani hapo uwanja wa amani mjini
Zanzibar.
(PICHA KWA HISANI YA BLOG YA VIJIMAMBO)
Na Ramadhani Ali- Maelezo Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka vijana wa
Zanzibar wabadilike na kujenga Utamaduni wa Ujasiriamali na wawe tayari
kujiajiri kupitia vyama vya ushirika vya uzalishaji mali pamoja na
kuanzishsa SACCOS ili kupata mitaji yenye unafuu.
Balozi
Seif ameeleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za
Wafanyakazi Duniani (Mei mosi) zilizofanyika katika Kiwanja cha Amaan na
kuwashirikisha Wafanyakazi wa Mawizara, Maidara na Mashirika ya
Serikali pamoja na taasisi binafsi baada ya kuyapokea maadamano ya
wafanyakazi hao.
Amesema
pamoja na Serikali kuchukua juhudi kubwa ya kupunguza tatizao la
ukosefu wa ajira kutoka asilimia saba mwaka 2007 hadi asilimia nne
mwaka 2010 bado tatizo la ajira ni changamoto kubwa Zanzibar kama
lilivyo nchi nyingi Duniani.
Hata
hivyo Makamu wa pili wa Rais ameahidi kwamba Serikali itaendelea
kufanya kila juhudi kupunguza ukosefu wa ajira nchini ili vijana waweze
kuishi kwa amani.
“La
muhimu vijana wetu waache tabia ya kuchagua kazi. Kazi ni kazi mradi
inakupatia riziki yako kwa njia ya halali, ” amesisitiza Balozi Seif Ali
Iddi.
Ameviagiza
Vyama vya Wafanyakazi kusaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa
njia ya kutoa elimu itakayowasaidia kukabiliana na ushindani wa soko la
ajira la sekta binafsi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Amesema
uzoefu unaonyesha kwamba vijana wengi wamekosa Utamaduni wa
kufanyakazi katika sekta binafsi, matokeo yake huacha kazi baada ya
kipindi kifupi cha kuajiriwa na nafasi zao kuchukuliwa na vijana kutoka
nchi jirani.
Makamu
wa pili wa Rais pia amevitaka vyuo vikuu nchini kuangalia mahitaji ya
ajira yaliyokuwepo nchini kwa kuandaa mitaala na mafunzo
yatakayowasaidia vijana kuajiriwa kwa urahisi.
“Vyuo
vyetu vikuu nchini navyo vinanafasi kubwa ya kusaidia kupunguza tatizo
la ajira kwa kuandaa mitaala yao ya kufundishia na mafunzo mengine kwa
mujibu wa mahitaji yaliyopo kama vinavyofanya vvyuo vikuu vyengine
vingi Duniani, ” alifahamisha Makamu wa pili wa Rais.
Blozi
Seif amewahakikishia wafanyakazi kwamba Serikali itaendelea kuchukua
hatua mbali mbali za kuboresha maslahi yao ili kuhakikisha yanalingana
na kazi wanazofanya na kwa upande wao amewataka kufanya kazi kwa bidii
na maarifa ili kukuza tija huku wakijua kwamba haki na wajibu ni watoto
pacha.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo Mwakilishi wa Shirika la kazi duniani (ILO)
Bibi Hopholang Phororo ameishauri Serikali kuendelea kuwajengea
wafanyakazi mazingira bora ya kazi ikiwemo kulinda afya na haki zao.
Ameahidi
kuwa Shirika hilo liko tayari kuendelea kuunga mkono katika kusaidia
juhudi za Serikali ili kuhakikisha wafanyakazi wako salama wakiwa
kazini.
Katibu
Mkuu wa ZATUC Maalim Khamis Mwinyi Muhammed ameelezea kuridhishwa na
mafanikio makubwa katika awamu ya saba ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kuwa karibu sana na Shirikisho hilo na kutekeleza kanuni na
sheria za kazi.
Hata
hivyo Maalim Khamis ameeleza masikitiko ya wafanyakazi wa Zanzibar kwa
kutopandishwa viwango vya mishahara yao mwaka uliopita licha ya uchumi
kuelezwa kuwa umekua.
0 comments:
Post a Comment