KAMATI
ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kimetangaza kuanza kwa Ligi ya vijana walio chini ya umri wa miaka 15,
itakayoanza Julai 29mwaka huu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa DRFA, Joseph Kanakamfumu, alisema jana baada ya kikao cha kamati hiyo, kilichokutana jana (Jumapili) kwenye Ukumbi wa Harbours Club Kurasini kuwa ligi hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho katika kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam unaibua vipaji kwa faida ya mkoa na Taifa.

Ligi hiyo itakuwa na faida kubwa
kutokana na kuenda sawa na umri unaotumika na mashindano ya vijana ya
Copa Coca Cola, ambayo mwaka huu yameanza kwa kushirikisha umri wa miaka
15.
Pia alisema ligi ya wanawake itaanza Agosti mwaka huu huku akiomba wadhamini nao kujitokeza kusaidia ligi hizo.
Wakati huo huo fomu kwa ajili ya
kozi ya waamuzi na ile ya mpira wa miguu kwa ngazi ya cheti cha pili
(Inter-Mediate) na zinapatikana kwenye ofisi za vyama vya mpira vya
wilaya vya IDFA, KIFA na TEFA.
0 comments:
Post a Comment