Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com, Soka In Bongo
SPURS KUCHEZA EUROPA LIGI!
SIR ALEX AAGWA KWA SARE YA 5-5 NA WBA!!
RVP ATWAA BUTI LA DHAHABU!!
BPL,
Barclays Premier League, leo imemaliza Msimu wake wa 2012/13 kwa
kukamilisha idadi ya Timu 4 za kucheza UCL,UEFA CHAMPIONZ LIGI, Msimu
ujao kwa Chelsea na Arsenal kuungana na Mabingwa Manchester United na
Manchester City na kuitupa Tottenham kucheza EUROPA LIGI.
Kabla
ya Mechi za leo tayari alishapatikana Bingwa ambaye ni Man United na
Mshindi wa Pili ni Man City na Timu zilizoshushwa Daraja ni Wigan, QPR
na Reading.
Kilichobaki
kilikuwa kinyang’anyiro cha Nafasi za 3,4 na 5 ambapo Chelsea
imefanikiwa kukamata ya Pili na Arsenal ya 4 hivyo kucheza UCL lakini
Chelsea, pamoja na Man United na City, zitacheza Makundi, na Arsenal
kuanza hatua ya Raundi ya Mchujo na ikifuzu itaingia Makundi.
Tottenham, kwa kumaliza Nafasi ya 5, itacheza EUROPA LIGI kuanzia Hatua ya Mchujo.
Katika
Mechi 10 za leo Jumla ya Mabao 36 yalifungwa huku Mechi ya mwisho kwa
Sir AlexFerguson akiwa Meneja wa Man United kumalizika kwa sare ya Bao
5-5 walipocheza ugenini na West Bromwich Albion ambayo pia
ilimuhakikishia Straika wao hatari Robin van Persie alieifungia Man
United Bao moja hii leo akimaliza Msimu akiwa na Bao 26 na hivyo
kunyakua Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora wa BPL Msimu huu.
Van Persie anafuatiwa na Luis Suarez wa Liverpool mwenye Bao 23 na Gareth Bale wa Tottenham mwenye Bao 21.
MATOKEO:
Jumapili 19 Mei, Chelsea 2 Everton 1, Liverpool 1 QPR 0, Man City 2
Norwich 3, Newcastle 0 Arsenal 1, Southampton 1 Stoke 1, Swansea 0
Fulham 3, Tottenham 1 Sunderland 0, West Brom 5 Man United 5, West Ham 4
Reading 2 na Wigan 2 Aston Villa 2
NIMEMALIZA
KAZI YANGU: Sir Alex Ferguson akiwatazama mashabiki wa united na
kuwaonesha ishara ya kwaheri baada ya kustaafu kuifundisha klabu hiyo
huku David Moyes akirithi mkioba yake
ANASEPA ZAKE: Ferguson akipanda basi la timu kwa mara ya mwisho akiwa meneja wa United
Fergie akiwatukuza mashabiki wa United waliosafiri kuwafuata West Brom
Mashabiki wa United wakionesha muda kuwa David Moyes amekaribishwa Old Trafford
David
Moyes ndivyo alivyoonekana leo baada ya kupoteza mchezo wa mwisho kwa
kufungwa mabao 2-1 na Chelsea, amemaliza muda sasa anakwenda United
KWAHERI: Ferguson alipewa heshima yake na timu zote kabla ya mechi kuanza
0 comments:
Post a Comment