Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kiungo
gwiji wa klabu ya Chelsea, wazee wa London, Frank James Lampard amesema
mchezaji mwenzake mkongwe wa klabu hiyo na nahodha John Terry atafuata
nyayo zake kwa kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo.
Kiungo
huyo wa timu ya taifa ya Uingereza aliongezewa mkataba wa mwaka mmoja
kukaa darajani baada ya kuvunja rekodi ya Bobby Tambling kwa kufunga
mabao mengi zaidi ambayo kwa sasa ni mabao203.
John
Terry aliyesumbuliwa sana na majeruhi msimu uliopita, hakuwa na nafasi
katika kikosi cha kwanza kocha mpya wa klabu hiyo Rafa Benitez.
Lampard ameliambia gazeti la The Sun kuwa ” najua JT anataka kuendelea kukaa Chelsea, anaipenda sana klabu yake na anajisikia vizuri kukaa hapa kama mimi”.
Lampard
na Terry ni malejendari wa Chelsea na wameisadia kutwaa ubingwa ligi
kuu mara tatu, ligi ya mabingwa barani ulaya, ligi ya Uropa, kombe la FA
na kombe la Ligi, hivyo Lampard anaamini mchango wao katika klabu yao
ni mkubwa sana na watabaki klabuni hapo.
Frank Lampard (kushoto) wakiwa zao ziarani nchini Marekani kujiandaa na msimu wa ligi kuu England.
NI NOMA TUPU: John Terry amekuwa katika wakati mgumu sana msimu uliopita na chini ya kocha Rafa Benitez amekalia benchi mno
0 comments:
Post a Comment