Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kiungo
mkongwe na kipenzi cha mashabiki wa timu ya taifa ya Engaland na klabu
ya Chelsea ya jijini London, Muingereza Frank James Lampard amesema
kamwe hajawahi kuwa na mahusiano ya karibu sana na kocha wa muda wa
klabu hiyo anayemaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu, Rafa
Benitez.
Rafa
aliyechukua mikoba ya aliyekuwa kocha kipenzi kwa mashabiki wa Chelsea,
Roberto Di Matteo ambaye alifukuzwa mwaka jana na mmiliki wa klabu hiyo
Roman Abramovich anasemekana kutokuwa na tabia ya kuwa na mahusiano ya
karibu sana na wachezaji wake.
Leo
hii kiungo Lampard ameeleza kuwa kocha huyo ambaye amekuwa akipingwa na
mashabiki wa klabu hiyo katika muda wake aliokaa klabuni hapo, kamwe
hajawahi kuwa na mahusiano na yeye pamoja na wachezaji wote wa Chelsea.
“Siku
zote Benitez amekuwa mtu wa mapambano na kujituma sana, ana uvumilivu
mkubwa sana, binafsi sijawahi kuwa chanzo cha yeye kuwaza vibaya, lakini
kitendo cha mashabiki wetu kumpinga ni udhaifu wa kibinadamu,
anatakiwa kuwasamehe”. Alisema Lampard.
Lampard
aliongeza kuwa kuna makocha ambao unaweza kuwa na mahusiano ya karibu
na kujihisi kama mtu wako wa karibu kwako, lakini Rafa huyuko hivyo
kwani anapenda zaidi kufanya mambo yake.
“Kiukweli sio kocha wa kukaa naye chini mkaongea”. Alisema Lampard.
Nyota
huyo alimsifu Benitez kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuandaa timu kwa
ajili ya mechi na kumfananisha na kocha Fabio Capello aliyekuwa kocha wa
timu ya taifa ya Uingereza “Simba watatu”.
Benitez
amewapa Chelsea ubingwa wa ligi ya Uropa na kufuzu kucheza ligi ya
mabingwa msimu ujao, lakini mkataba wake unaisha mwishoni mwa mwezi huu.
Frank Lampard amesema hajawahi kuwa na mahusiano ya karibu na kocha wake Rafa Benitez
Lampard amepewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja darajani baada ya kuwepo kwa wasiwasi mkubwa kuwa angemalizana na klabu hiyo
Nyota huyo mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuifungia Chelsea mabao mengi zaidi ambapo mpaka sasa ametia kambani mabao 203 huku akitarajiwa kuichezea klabu yake chini ya kocha Jose Mourinho msimu ujao.
Nyota huyo mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuifungia Chelsea mabao mengi zaidi ambapo mpaka sasa ametia kambani mabao 203 huku akitarajiwa kuichezea klabu yake chini ya kocha Jose Mourinho msimu ujao.
Benitez amefanikiwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa na kutwaa kombe la Uropa mwaka huu
MKATABA MPYA: Lampard ameongezewa mkataba mpya wa mwaka mmoja kuichezea Chelsea
0 comments:
Post a Comment