Na Baraka Mpenja
Mwenyekiti
mpya wa chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Anna Kibira amesema,
uongozi mpya wa chama hicho unarajia kuhamasisha mchezo huo uchezwe kila
kona ya mipaka ya Tanzania na watu waliopewa vipaji na mungu
walitumikie taifa kwa dhati yao.
Kibira
ameiambia MICHEZO! kutokea jijini Mbeya kuwa mipango yao ni kupata
vijana wengi wenye vipaji maeneo mbalimbali ya taifa hili lilijaa vipaji
katika michezo na kuunda timu tatu za taifa.
“Tunataka
netiboli iwe mchezo mashuhuri zaidi, vijana wote wa Tanzania wapate
nafasi ya kucheza, tukifanya hivyo tutakuwa na timu nzuri za taifa na
sasa tunataka kuwa na timu tatu, yaani ya vijana wadogo, wakati na watu
wazima”. Alisema Kibira.
Mwenyekiti
huyo alisema mpaka sasa hawajakabidhiwa rasmi ofisi, lakini wiki mbili
zijazo watakabidhiwa na baada ya hapo watakaa kikao cha kwanza ili
kupanga mikakati yao na kuangalia kalenda yao imekaaje.
Kibira
aliongeza kuwa watanzani wawe na imani na uongozi mpya kwani
wanajipanga kuendeleza mambo mazuri ya uongozi uliopita chini ya
mwenyekiti wake Anna Bayi.
“Nafikiri
tunayo kazi ya kufanya mengi zaidi ya uongozi uliopita, tunakuja na
sera mpya ya kuufanya mchezo wa Netiboli Tanzania uwe wa kuvutia zaidi
na kupeperusha bendera ya taifa kimataifa”. Alisisitiza Kibira.
Akizungumzia
hali ya wadau kuwa nyuma kuthamini mchezo wa Netiboli, Kibira alisema
lazima watanzania wakumbuke kuwa mchezo huo umelipa taifa sifa kubwa
hasa baada ya timu ya taifa “Taifa Queens” Kufanya vizuri medani ya
kimataifa.
“Imefika
wakati wa kutukumbuka CHANETA, tuna mikakati mizito sana na tunahitaji
uwezeshaji mkubwa sana, tunawaomba watanzania kutuunga mkono sana kwa
kutuchangia na kuwekekeza katika mchezo huu”. Alisema Kibira aliyeshinda
uchaguzi wa CHANETA aprili 20 mwaka huu.
Michezo
sio soka tu, makampuni yanayojitokeza kudhamini mchezo wa soka
yakumbuke pia kujiingiza katika mchezo wa Netiboli kwani unaweza
kulitangaza vizuri taifa medani ya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment