Tuesday, May 28, 2013

Vieira © Action Images

 
 
Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Supersport.com
 
Kocha wa miamba ya soka la Misri, Zamalek Jorvan Vieira ametangaza kuondoka baada ya mkataba wake kumalizika mwezi juni mwakani.
 
Vieira alijiunga na Zamalek mwezi juni mwaka jana baada ya kuondoka kwa kocha wa zamani wa klabu hiyo Hassan Shehata.
 
“Nina wakati mgumu sana nchini Misri, sasa nina sababu zangu binafsi za kuondoka baada ya mkataba wangu kumalizika mwezi juni mwakani”.
Alisema Vieira ambaye klabu yake ilipoteza mchezo siku chache zilizopita dhidi ya Ittihad katika michuano ya ligi kuu ya Misri.
 
Kocha huyo aliendelea kusema kuwa “Familia yangu iko mbali na mimi, nahitaji kuwa nao. Wao ndio kila kitu kwangu na hii ndio sababu kubwa ya mimi kutaka kuondoka Misri”.
 
Tetesi za chini zilieleza kuwa Vieira anataka kujiunga na wapinzani wakubwa wa Zamalek, klabu ya Al Ahly, lakini alisema “Hiyo sio kweli, haina maana kuihama Zamalek na kujiunga na Ahly, nimepata ofa nyingi sana kutoka nchi za kiarabu ila Al Ahly sio mojawapo”.
 
Ripoti nyingine zinaonesha kuwa kocha huyo mwenye miaka 60 anataka kutimkia Kuwait na kuwa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video